Mratibu
wa Mradi wa Madhara ya Tumbaku (TPHA) Dk. Bertha T.A. Maegga
akizungumza wakati akifungua kongamano hilo lililo washirikisha wadau
mbalimbali kwa kutoa muhutasari wa Madhara ya Tumbaku. (Picha na Geofrey
Adroph).
Na Andrew Chale, modewjiblog[Dar es Salaam] Chama cha Afya ya Jamii nchini (TPHA), kimeendesha kongamano maalum kwa wanafunzi wa shule msingi zaidi ya Saba ndani ya Manispaa ya Kinondoni kwa lengo la kutoa elimu ya madhara yatokanayo na utumiaji wa bidhaa za Tumbaku pamoja na kujikinga na athari zake mbaya baadae.
Akielezea katika kongamano hilo, Afisa wa TPHA ambaye pia ni msimamizi na mtaafiti wa masuala ya kupambana na madhara ya Tumbaku, Dk. Bertha Maegga amebainisha kuwa, kwa sasa Chama hicho kinaendesha mradi uliopewa jina la “80 CHILDREN STRONG” ukitoa elimu kwa vijana wadogo wenye umri wa miaka 10-14, hasa wa shule za msingi.
Dk. Maegga akihutubia umati wa wanafunzi wa shule hizo saba katika kongamano hilo lililofanyika shule ya Msingi Kijitonyama Visiwani, aliwataka wazazi, walimu, walezi na jamii kuwalinda na kukemea watoto wao kuachana na vitendo vya matumizi ya bidhaa za Tumbaku ikiwemo sigara, ugoro, shisha na Tumbaku yenyewe.
Aidha, amebainisha kuwa, wameweza kulenga kundi hilo kutokana na kuwa na changamoto za kiukuaji wa kiakili na kisaikolojia.
“Umri huu kuna utundu na utukutu mwingi na akili nazo bado hazijakomaa kuepuka ushawishi wa namna mbalimbali ukiwemo na wa matendo yasiyofaa katika maisha yao ya baadaye.
Tukiweza
kuwalinda katika umri huo. watabaki salama hadi watakapojitambjua nafsi
zao na kuamua mambo ya busara na salama katika maisha yao ya baadae”
alibainisha Dk. Maegga.
Mshauri wa masuala ya Afya na Familia, mgeni rasmi Dk. Ali Mzige akizungumza kwa kutoa elimu kwa miongoni mwa watu walio weza kuhudhuria kongamano hilo la uelimishaji kuhusu Tumbaku na matumizi ya yanayotokana na bidhaa za Tumbaku.Kwa upande wake, Dk. Ali Mzige mganga wa hospitali ya kimataifa ya Afya ya uzazi ametoa elimu kwa vijana hao na kubainisha kuwa sigara, tumbaku, shisha, ugoro na kuberi ni hatari kwa afya za mwili huku ikisababisha magonjwa mbalimbali.Miongoni mwa magonjwa hayo yatokanayo na matumizi ya sigara ambapo wanaoathirika zaidi ni vijana kwa sababu ya kufuata mkumbo pamoja na kuhisi kwamba uvutaji wa sigara unaongeza sifa ya kuwa mwanaume kamili kitu ambacho si kweli.Changamoto kubwa ni kwamba serikali imeshindwa kudhibiti watengenezaji wa Sigara kwa sababu wanapata kodi kutoka katika viwanda vya sigara japokuwa mapato ni madogo kuliko madhara.“Sigara ina kemikali 4000 ambazo zina uwezo wa kusababisha magonjwa zaidi ya 40, ambayo ni pamoja na ugonjwa wa moyo, kisukari, na saratani ya mapafu, saratani ya kinywa na mengine mengi.
Tumbaku na Sigara zote zimekuwa na madhara yanayofanana. Tumbaku imekuwa ikitumika hasa maeneo ya vijijini na sigara watumiaji wengi wanatoka mjini” alieleza Dk. Ali Mzige.
Kwa
upande wao wanaharakati wa kupambana na matumizi ya sigara kutoka chuo
cha Tiba Muhimbili, kupitia taasisi yao ya African Fight Cancer,
Bernard Temba amewaelezea wannafunzi hao kuwa, ni wakati wa kuepuka
vishawishi dhidi ya watu wanaotumia sigara kwani wasipofanya hivyo
wataweza kupata madhara makubwa ya kiafya.
Mwalimu
Margareth William mshereheshaji katika siku hiyo ya kongamano la
uelimishaji vijana kuhusu Tumbaku na madhara yatokanayo na bidhaa zake.
Naye
Mratibu wa Elimu Kata ya Makumbusho ambaye pia alikuwa mgeni katika
kongamano hilo, alitoa wito kwa walimu na wazazi kuwa waangalifu kwa
watoto wao ikiwemo kufuatilia nyendo zao mara kwa mara ili kuwakinga na
vishawishi hivyo vya matumizi ya bidhaa zitokanazo na tumbaku kwani
zina madhara makubwa hasa kwa afya za watoto wadogo.
Mradi
huo wa ’80 Children Strong’, unaosimamiwa na Chama cha Afya ya Jamii
(TPHA) unafadhiliwa na Shirika dogo la Conquer Cancer Foundation
ambalo linahusiana na American Society for Clinical Oncology (ASCO)
ya nchini Marekani (Chama cha kitabibu cha masuala ya uchunguzi wa tiba
ya saratani.
Hata
hivyo, TPHA imedhamiria kuwa kila mtoto anapata haki ya kuelimishwa
kujikinga na matumizi hayo mabaya ya tumbaku, ambapo kwa darasa la
watoto 80, asiwepo hata mmoja atakayeingia kwenye viashiria vibaya vya
matumizi ya tumbaku hivyo wataendelea kutoa elimu hiyo sehemu
mbalimbali nchini.
Kwa
upande wa shule hizo zilizohudhuria kongamano hilo ni pamoja Shule ya
Msingi Mapambano, Kijitonyama Visiwani, Victoria, Mwananyamala B,
Mwananyamala Kisiwani, Mashujaa, Shekilango na Mapambano.
Kwa
upande wa watoto hao walipata pia wasaha wa kuuliza maswali na kupatiwa
majibu huku pia kukifanyika na masuala ya maigizo, ngoma, shahiri na
ngonjera zilizokuwa na jumbe mbalimbali za kupambana na matumizi ya
tumbaku.
Wanafunzi wakisoma na kuelekezana jarida lililochapishwa mahususi kwa ajili ya kuelimisha matumizi mabaya ya Tumbaku.
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka mashirika na vyuo mbalimbali.
Kikundi
cha majigambo ya jukwaani (ngonjera) kikitoa ujumbe kwa wageni waalikwa
pamoja na wanafunzi wenzao kuhusiana na kupambana na kudhibiti matumizi
hatari ya Tumbaku.
Wanafunzi
wakionesha vipaji vyao vya kuigiza kwa kuelimisha kuhusiana na na
madhara ya Tumbaku na ni namna gani ya kuweza kujikinga.
Bernard
Temba kutoka Chuo cha Afya cha Muhimbili akitoa somo kwa wanafunzi wa
shule za msingi zilizohudhuria kongamano hilo lililofanyiaka katika
shule ya Msingi ya Kijitonyama Kisiwani
Shairi
mahususi likiimbwa na wanafunzi hao likiwa limebeba ujumbe wa kijana
jiepushe na matumizi ya Tumbaku na bidhaa zitokanazo na Tumbaku.
Mwanafunzi
wa darasa la tano, Tadei Ladislausi kutoka shule ya msingi Shekilango
(kulia)akisoma madhara yanayo wakumba watumiaji wa Tumbaku.
Wawili
kulia ni wanafunzi kutoka Chuo cha Afya Muhimbili, kushoto ni wanafunzi
wa shule ya msingi Kijitonyama Kisiwani wakiwa wanasikiliza kwa makini
maada zilizo kuwa zikiendelea katika kongamano hilo.
Wanafunzi wakiuliza maswali kwa watoa mada inayo husiana na afya kwa kijana na kuepuka matumizi mabaya ya Tumbaku
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kijitonyama Kisiwani, Bw. Charles Nombo akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wanafunzi.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali walioweza kuhudhuria katika kongamano hilo.
Mjumbe
wa Chama cha Afya ya Jamii Bi. Elizabeth Nchimbi akitoa nasaa kwa
vijana walioweza kuhudhuria na wale walioko nje wasiweze kutumia Tumbaku
kwani ni hatari kwa afya za binadamu
Waandhishi wa habari wakiwa kazini.
Afisa
Elimu kata ya Kijitonyama, Mwalimu Shangwe Temba akifunga kwa kutoa
neno kwa vijana kuacha kujiingiza katika makundi mbalimbali kwani ndio
yanayo pelekea vijana wengi kuhamasika na kuanza kutumia Tumbaku ambayo
huwaletea vijana wengi matatizo hususani kwa wanafunzi kuacha shule kwa
kuugua vifua vikuu na magonjwa mengine mengi
Picha ya umoja wa kikundi cha wanafunzi kinacho elimisha matumizi mabaya ya bidhaa zinazotokana na Tumbaku.
No comments:
Post a Comment