Ni
siku ya 14 ambapo mampema kabisa washiriki wa shindano la Mama Shujaa
wa Chakula Msimu wa nne 2015 linaloendeshwa na Oxfam kupitia kampeni
yake ya Grow na yenye kauli yake ya Wekeza kwa wakulima wadogo wadogo
wanawake inalipa , na Kipindi ambacho kinaruka katika Runinga yako
kupitia Chanel ya ITV kuanzia saa 12:30 jioni na Marudio saa 11:30 za
asubuhi , Katika siku hii Mama Shujaa wa Chakula wanatoka na kuelekea
mabondeni kufuata udongo wa Mfinyanzi kwa ajili ya kuja kutengeneza vitu
mbalimbali kama majiko, Mifuniko, Mabanda, mapambo, Vyungu na vitu
vyengine vingi.
Ilikuwa
ni Safari ndefu ya kufuata udongo huo lakini hatimaye walifanikiwa
kuupata na baadae kurudi katika Kijiji chao cha Kisanga na kuanza
kutengeneza vitu hivyo na baadae kuwauzia wanakijiji wa Kijiji cha
Kisanga.
Pia
hii ilikuwa ni nafasi kubwa na ya kipekee kwa Washiriki hao wa Shindano
la mama Shujaa wa Chakula kuuza vitu vyao ambavyo walitengeneza wakiwa
kwao pamoja na Bidhaa mbalimbali kwa wakazi wa Kijiji cha Kisanga...
Hivi ndivyo ilivyokuwa.
Mama
Shujaa wa Chakula wakiwa wanaelekea Bondeni katika kijiji cha Kisanga
kufuata udongo wa Mfinyanzi kwa ajili ya kutengeneza vitu mbalimbali
ambavyo viliwasaidia kupata kipato.
Washiriki
wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa nne 2015 Shindano linalo
endeshwa na Oxfam kupitia Kampeni yake ya Grow wakiwa wanachimba udongo
wa Mfinyanzi kwa ajili ya kwenda kutengeneza vitu mbalimbali ambavyo
baadae waliviuza
Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 msimu wa nne wakiwa wanamalizia kuchimba udongo
Kazi
imeanza ambapo washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa chakula linalo
endeshwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow na Kurushwa katika
Runinga yako kupitia Chanel ya ITV kuanzia saa 12:30 za jioni na
Kurudiwa saa 11:30 asubuhi wakiwa bize kila mtu kufinyanga vitu
mbalimbali
Kila mmoja yupo bize kutengeneza kitu chake
Kazi inaendelea ambapo mmoja wa washiriki anaonekana akitengeneza kitu chake kwa ustadi mkubwa
Hiki kikiwa katika hatua za mwisho
Mmoja wa washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 akiwa anamalizia kutengeneza kitu chake kwa umakini Mkubwa
Wakiendelea kufinyanga vyungu
Wakiendelea kukamilisha kutengeneza vyungu pamoja na Majiko kwa kutumia udongo wa mfinyanzi
Sasa
kila kitu kimekamilika washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula
2015 wakiwa wameweka bidhaa zao ambazo wamezitengeneza kijijini pale na
zengine wametoka nazo makwao kwa ajili ya kuziuza kwa wanakijiji wa
Kisanga
Baadhi
ya wanakijiji wa kijiji cha Kisanga wakiwa wamefika katika sehemu
ambayo akina mama shujaa wa chakula walikuwa wanauza vitu vyao ambavyo
walitengeneza kijijini hapo na vyengine walitoka navyo makwao na
kuvinunua.
No comments:
Post a Comment