Marafiki
wa Wafanye Watabasamu, hivi karibuni, walitembelea kituo cha watoto
yatima (Amani Orphanage Centre) kilicho katika Kijiji cha Zinga,
Bagamoyo kwa ajili ya kutoa misaada mbali mbali kisha kuchora nao. Mbali
na marafiki waishio nchini, pia kulikuwa na walimu sita toka Shule ya
Msingi ya Catton Grove ya Uingereza na wawakilishi wa taasisi ya The
Tanzania Norwich Association pia ya Uingereza. (Picha: Nicolas Calvin).
Msafara wa Wafanye Watabasamu ukiwasili kituoni hapo. Zaidi kuhusu programu hii tembelea: https://www.facebook.com/wafanyewatabasamu.
Mkurugenzi
wa kituo cha Amani Orphanage Centre, Bi. Margareth Mwegalawa wa pili
toka kulia aliyesimama, akitoa taarifa fupi kuhusu kituo hiko.
Mratibu
wa Wafanye Watabasamu ambaye pia ni mchora vibonzo ITV, Nathan Mpangala
akiwashukuru marafiki mbalimbali waliochangia misaada na kufanikisha
ziara hiyo.
Sanaa ya uchoraji nayo ikachukua nafasi yake.
Mmoja wa watoto wa kituo hiko akijitambulisha kwa wageni.
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo hiko wakifurahi na wageni waliowatembelea. Kituo hiko kina watoto 37.
Watoto wa Kituo cha Amani Orphanage Centre walimwaga shoo ya nguvu kwa wageni.
Baadhi ya marafiki wa Wafanye Watabasamu wakijiachia na watoto.
Baadhi ya watoto na marafiki wa Wafanye Watabasamu wakionesha kazi zao.
Naam, raha ya shughuli mlo bwana.
No comments:
Post a Comment