Bendi
mpya ya muziki wa dansi ijulikanayo kama The Stars Band iliyo chini ya
Aneth Kushaba imezinduliwa rasmi siku Jumamosi ya Julai 18, siku ya
Idd-Mosi ndani ya kiota cha Mzalendo Pub, Kijitonyama jijini Dar es
Salaam huku ikisindikizwa na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya
Barnabas pamoja na bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.
Mkurugenzi
wa The Stars Band, Aneth Kushaba akijitambulisha kwa mashabiki wakenm
pamoja na azungumza na wapenzi wa bendi mpya ya The Stars Band wakati wa
uzinduzi yeye binafsi alisema hawezi kusema yaliyopita bali wapenzi wa
bendi hiyo wategemee makubwa kutoka kwenye bendi hiyo iliyozinduliwa
siku ya Idd Mosi ndani ya kiota cha Mzalendo Pub.
Mwimbaji
wa Bendi ya The Stars, Felly Kano akionesha mambo yake kwenye stage hii
yote ni wakati anajitambulisha kwa mashabiki wa bendi waliofika kwenye
uzinduzi wa bandi hiyo.
Mwimbaji
wa Bendi ya The Stars, Seghito mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangozi
akijitambulisha kwa kuonesha uwezo wake kwenye stage wakati wa uzinduzi
wa bendi hiyo uliofanyika katika kiota cha Mzalendo Pub jijini Dar.
Mpiga Drums na pia ndiye meneja wa Bendi, Kibosho akijitambulisha kwa kuone uwezo wake katika Drums.
Mpiga la Gitaa katika Bendi ya The Stars, Othuman Majuto akionesha ujuzi wake kwenye stage wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo.
Mpiga la Gitaa la Base katika Bendi ya The Stars, Zaid Sato (Base) akionesha mambo yake kwenye stage.
Mpiga la Keyboard katika Bendi ya The Stars, Sebastian akionesha maujaja yake.
Mwimbaji
wa Bendi ya The Stars, Alawy Junior akijitambulisha rasmi wakati wa
Uzinduzi wa Bendi hiyo Mpya iliyojaa vipaji vya ukweli.
Mwimbaji
wa Bendi ya The Stars, Prince ambaye aliwavutia walembo wengi kutokana
na sauti yake wakati wa kujitambulisha wakati wa uzinduzi wa Bendi hiyo.
Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Mao Santiago akijitambulisha kwa kuimba sebene moja matata ilikuwa ni hatari
Mwimbaji
wa Bongo Flava, Barnaba Elias aka Barnaba akiimba moja ya nyimbo zake
huku akisindikizwa na waimbaji wa Bendi ya The Stars kutshoto ni Seghito
na kulia ni Prince
Mwimbaji
wa Bongo Flava, Barnaba Elias aka Barnaba akiendelea kutoa burudani
ndani ya kiota cha Mzalendo Pub wakati wa Uzinduzi wa Bendi mpya ya The
Stars iliyozinduliwa siku ya Idd - Mosi
Mwimbaji
wa Bongo Flava, Barnaba Elias aka Barnaba akiimba sambamba na Mwimbaji
wa Bendi ya The Stars, Alawy Junior wakati wa uzinduzi wa sendi mpya ya
The Stars
Waimbaji
wa Bendi ya The Stars wakiimba kwa pamoja wakati wa Uzinduzi wa Bendi
hiyo ndani ya Kiota cha Mzalendo Pub, KIjitonyama jijini Dar
Mwimbaji
wa Bendi ya The Stars, Seghito (wa pili kutoka kushoto) akiimba moja ya
nyimbo zinazobaba katika dunia hii huku akisindikizwa na waimbaji
wenzake amabo ni Felly Kano(wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Bendi,
Aneth Kushaba( wa pili kutoka kulia) pamoja na Prince (wa kwanza kulia)
Waimbaji
wa Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma' ambao ni Jesus(wa kwanza
kushoto) akifuatiwa na Patcho Mwamba(wa pili kutoka kushoto), Pablo
Masai (katikati), Mulemule(wa pili kutoka kulia) pamoja na 33 wote
wakiimba kwa pamoja wakati wa uzinduzi wa bendi mpya ya The Stars katika
kiota cha Mzalendo Pub
RAIS wa
bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma', Nyoshi El Sadat akiimba kwa
hisia kali wakati wa uzinduzi wa bendi ya The Stars iliyofanyika kwenye
kiota cha Mzalendo Pub siku ya Idd-Mosi
Wakati wa
uzinduzi wa Bendi ya The Stars ilikuwa ni funika mbayaaaaa maana Bendi
ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma ilifanya ya kwao
Waimbaji
wa Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma wakiongozwa na Totoo
Kalala(wa kwanza kusoto) pamoja na MP 3 (wa kwanza kuli) wakiendelea
kutoa burudani huku wakisindikizwa na waimbaji pamoja na wanenguaji wa
bendi hiyo
Ni burudani kwenda mbele
Wanenguaji
wa bendi ya Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma wakiendelea kutoa
burudani wakati wa uzinduzi wa bendi mya ya The Stars
Waimbaji
wa Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma wakiongozwa Rais wa bendi
hiyo, Nyoshi El Sadat wakiendelea kutoa burudani wa wapenzi wa bendi ya
FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma pamoja naThe Stars Bandi
Mwimbaji
wa Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma wakiongozwa, Totoo Kalala(wa
kwanza kusoto) akiendelea kuimba huku akisindikizwa na wanenguaji wa
bendi hiyo
Burudani ikiendelea
Waimbaji
wa Bendi ya The Stars wakendelea kutoa burudani wakati wa uzinduzi wa
bendi hiyo uliofanyika siku ya Idd Mosi katika kiota cha Mzalendo pub
Wakiendelea kucheza kwa furaha wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo
Mwimbaji
wa Bendi ya The Stars, Felly Kano(wa pili kutoka kulia) akiimba kwa
hisia kali huku akisindikizwa na na waimbaji wenzake ambao ni Mao
Santiago(wa kwanza kushoto), Seghito (wa pili kutoka kushoto) pamoja na
Mkurugenzi wa Bendi ya The Stars, Aneth Kushaba
Mkurugenzi
wa Bendi ya The Stars, Aneth Kushaba(kushoto) akiimba na Mwimbaji wa
Bendi ya The Stars, Felly Kano ambao kwa pamoja wameamua kuitumia fursa
walioipata kupitia vipaji vyao vya kuimba.
Waimbaji
wa Bendi ya The Stars wakiendelea kutoa burudani mbele ya mashabiki wao
(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo uliofanyika siku ya
Idd Mosi atika kiota cha Mzalendo Pub jijini Dar
Mkurugenzi
wa Bendi ya The Stars, Aneth Kushaba(kushoto) akiimba na Mwimbaji
mwenzake wa Bendi ya The Stars, Seghito wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo
Mwimbaji
wa Bendi ya The Stars, Mao Santiago( wa pili kutoka kushoto) akiendelea
kuimba sebene za nguu uku akisindikizwa na waimbaji wenzake ambao ni
Seghito(wa kwanza kushoto), Felly Kano (wa pili kutoka kulia) pamoja na
Alawy Junior(wa kwanza kulia)
Ndani ya Bendi mpya ya The Stars ni full burudani na sio chenga
The Stars Band wakiendelea kutoa burudani
Mwimbaji
wa Bendi ya The Stars, Alawy Junior(kushoto) akiimba sambamba na
Mkurugenzi wa Bendi ya The Stars, Aneth Kushaba(kushoto) wakati wa
uzinduzi wa bendi hiyo uliofanyika siku ya Idd-Mosi katika kiota cha
Mzalendo Pub, Kijitonyama jijini Dar
Ndani ya
bendi ya The Stars ni full raha hapa waimbaji wa bendi hiyo wakionesha
moja ya style yao kwa mashabiki waliofika kwenye uzinduzi huo
Mashabiki wa Bendi ya The Stars wakiendelea kuserebuka na ngoma za bendi hiyo wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo
Waimbaji wa Bendi ya The Stars wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo
Wazee wa kusababisha hara za mziku zinakua poa kutoka katika bendi ya The Stars wakiwa kwenye picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment