Mjumbe wa Baraza la Michezo la Tanzania Bara
(BMT), Jamal Mandenda Rwambow (pichani) amerejesha fomu kuwania Ubunge wa Jimbo la Rufiji
klupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza jijini jana, Rwambow ambaye ni mdau mkubwa wa
michezo alisema kuwa sababu kubwa ya kuomba kuwatumikia wakazi wa jimbo la
Rufiji ni kuleta maendeleo ya haraka katika kila sekta.
Alisema kuwa mbali ya sekta ya michezo, pia amepania
kuwakwamua wakaji wa jimbo hilo katika hali ya umaskini waliyokuwa nayo hasa
kwa kutumia utajiri wa rasilimali za jimbo hilo ikiwemo bonde la kilimo la mto
Rufiji.
Alifafanua kuwa pamoja na kuweka nia ya kutekeleza ilani ya
Uchaguzi ya CCM, pia ameweka vipaumbele kadhaa ambavyo ndivuo vitawafanya
wakazi wa jimbo hilo kupata maendeleo ya kina na si vinginevyo.
“Kwenye michezo nitasaidia timu na kuinua vipaji na
kuviendeleza na kufikia hatua ya juu kabisa, jimbo la Rufiji lina wachezaji
wengi wa mpira wa miguu, mpira wa kikapu, netiboli na michezo mingine, hata
mabondia wapo katika jimbo hilo, hakuna mtu aliyeweza kuwatoa hapo walipo na
kufikia kiwango cha kitaifa na kimataifa, kazi hiyo sasa itakuwa ya kwangu
mimi,” alisema Rwambow.
Alisema kuwa aliwajengea uzio wa uwanja wa mpira wa miguu,
hatua ambayo iliwawezesha wachezaji kuanza kufaidi matunda ya uchezaji wao
baada ya kuanza kupata fedha kidogo kutokana na jasho lao.
Kuhusiana na sekta nyingine, Rwambow alisema kuwa nyenzo kuu
ni kutafuta mitaji, kuweka mipango na kuitekeleza, kufanya kazi kama timu moja,
kuyafanya mambo ya maendeleo kwa haraka zaidi na kutambua watendaji bora na
kuwakemea wazembe.
“Nitahakikisha tunafanyakazi pamoja kwa vitendo na siyo
kusema tu, hii itakuwa katika sekta zote ambazo ni muhimu kwa binadamu,”
alisema.
No comments:
Post a Comment