Mtaalamu
wa Mradi wa Kilimo chenye tija Tanzania (TAPP ), Mussa Madurufu (
anayenyosha mikono) akitoa elimu ya namna ya kuendesha wa kilimo cha
bustani ya nyanya kwa njia ya teknolojia mpya ya umwagiliaji kwa njjia
ya matone wakati wa maadhimisho ya siku ya wakulima Julai 20, 2015
katika bustani ya vipando vya mboga na matunda ya Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo (SUA), maonesho yaliyodhaminiwa na Asasi kilele ya
sekta binafsi yenye lango kuu la kuhamasisha maendeleo ya kilimo cha
mazao ya horticulture Tanzania (TAHA),TAPP ,Mradi wa Tafiti Bunifu za
Kilimo (iAGRI), na SUA.
Ulaji wa matunda ni muhimu kwa afya ya mwili wa binadamu.
Baadhi
ya Wakulima waliokuwa wakihudhuria maonesho ya wakulima na teknolojia
mpya ya umwagiliaji kwa njjia ya matone wakipita kuangalia kipando cha
bamia , maonesho hayo yalifanyika julai 20, 2015 , SUA na
yalidhaminiwa na Asasi kilele ya sekta binafsi yenye lango kuu la
kuhamasisha maendeleo ya kilimo cha mazao ya horticulture Tanzania
(TAHA),TAPP ,Mradi wa Tafiti Bunifu za Kilimo (iAGRI), na SUA.
Mtaalamu wa kilimo kutoka TAPP akiangalia ustawi wa mboga aina ya spinach.
Mtaalamu wa lishe kutoka TAHA akiwaeleza wakulima faida ya kula matunda.
Wakulima wakipatiwa mafunzo ya kilimo bora cha matunda na mbogamboga.
Na John Nditi, Morogoro
NCHI
za Afrika Mashariki zimeanzisha mchakato wa kuweka viwango vya
ubora wa mazao ya kilimo cha bustani kinachohusisha matunda na
mboga mboga ukiwa ni mkakati wa kuwalinda walaji na pia kukidhi
ubora wa soko la nchi wananchama wa Jumuiya ya nchi hizo.
Hayo
yalisemwa na Makamu wa mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),
Profesa Gerald Monela , Julai 20,2015 wakati akifungua mafunzo ya
maonesho kwa wakulima ya teknolojia mpya kilimo cha umwagilijai kwa
njia ya matone cha bustani ambacho huchanganywa mbolea na maji kwa
wakati mmoja .
Maadhimisho
yao wakulima yalidhaminiwa na Asasi kilele ya sekta binafsi yenye lango
kuu la kuhamasisha maendeleo ya kilimo cha mazao ya horticulture
Tanzania (TAHA), Mradi wa Kilimo chenye tija Tanzania (TAPP)
unayofadhiliwa na Shrika la Misaada la Marekani (USAID), Mradi wa Tafiti
Bunifu za Kilimo (iAGRI), na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).
Wakulima
zaidi ya 100 wamehudhuria maonesho hayo ya teknolojia mpya ya
umwagiliaji kwa njjia ya matone ambapo walieeleza namna
watakavyonufaika na tekenolojia hiyo ingawa ina changamoto zake .
Kwa
mujibu wa Makamu wa mkuu wa SUA, sekta ya Kilimo cha bustani
‘Hotcultural’ inakuwa kwa kiwango cha hali ya juu na waliowekeza katika
kilimo hicho wameinuka kiuchumi.
“
Teknolojia mpya ya umwagiliaji wa matone katika kilimo cha ‘horticultre’
kina faida , lakini lazima kiwekewe viwango vya ubora ili kukidhi
soko ndani na nje ya nchi” alisema Makamu wa Mkuu wa SUA.
Kwa
mujbu wa Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, kupitia kitivo cha
horticulture kimeanzisha kituo ambacho kinatumika kufundisha wakulima
na wanafunzi kilimo hicho kwa kufundishwa teknolojia mbalimbali
ikiwemo cha kilimo hicho.
Pamoja
na hayo alitumia fursa hiyo kuiomba serikali kutengeneza mazingira
mazuri kwa kushirikiana na makampuni ili kupunguza bei za viuwatilifu,
pembejeo za kisasa pamoja na mbegu bora ili kuwawezesha wakulima wadogo
kumudu kuzinunua na kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo.
Kwa
upande wake Maneja Uhandisi Kilimo wa TAHA, Kitururu Mbwambo alisema
TAHA inatoa mafunzo mbalimbali yanayolenga kunjengea mkulima uwezo wa
kuzalisha mazao bora yenye viwango vinavyokubalika katika masoko.
Hata
hivyo alisema , mafunzo hayo ni pamoja na mbinu bora za kilimo kwa
kutumia teknolojia mbalimbali na pia yanalenga kuwajengea wadau uwezo
kwenye masuala ya biashara, namna ya kuendesha vikundi ama ushirika na
masuala ya fedha.
Meneja
huyo wa Uhandisi Kilimo TAHA, alizitaja shughuli nyingine ni kujenga
mazingira wezeshi ya biashara ya mazao ya horticulture, upatikanaji wa
fedha, huduma za usafirishaji wa mazao ya aina hiyo na kugamaisha
viwango vya mazao ya horticulture.
No comments:
Post a Comment