Balozi wa Simba Octa Mshiu akipokea Hati ya Ubalozi kutoka kwa Rais wa Simba Evans Aveva. Anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Eaggroup Imani Kajula
Dhima yetu ya kuendeleza mabadiliko ndani ya Simba bado inaendelea kushika kasi, Katika kipindi cha miezi mitatu sasa, mmekuwa mashuhuda wa Simba inayolenga kuleta mapinduzi makubwa katika jinsi mpira unavyoendeshwa, kujali wanachama, wapenzi wake na kukuza vyanzo vya mapato.
Akizungumza na waandishi wa habari Rais wa Simba Evans Aveva alisema ‘’Katika kukuza wigo wake wa kuwashirikisha wapenzi wake katika kuleta maendeleo ya klabu Simba Sports Club inazindua makakati wa kuwashirikisha wapenzi wenye nia ya kuwa chachu ya maendeleo kwenye klabu yao. Simba ni klabu ya wanachama na wapenzi wa Simba, hili ndilo jambo la msingi
malengo mbalimbali ya klabu ya Simba. Hivyo basi leo hii klabu ya Simba inazindua rasmi Mabalozi wa Simba, hawa ni wapenzi wa Simba ambao wako tayari kushirikiana na klabu katika kuleta maendeleo ya klabu yetu’’.
Aveva aliendelea kusema ‘’ Katika ahadi zetu wakati wa uchaguzi tuliahidi kuwa tumenuia kwa dhati kuleta mapinduzi ya kimaendeleo ndani ya Simba. Napenda kusema safari yakuendelea kuifanya Simba kuwa klabu bora ndani na nje ya uwanja imepamba moto. Kwa uhakika malengo mengii kiwemo la kujenga uwanja na kambi ya mazoezi ya Simba sio ndoto. Kupitia mabalozi wa Simba na mikakati yetu mingine ya utunishaji wa mapato tunaamini kwa dhati malengo yetu tutayafikia.
Kihistoria Simba imekua ni timu yenye kutendana kufikiriki maendeleo na kutumia nguvu za wapenzi na wanachama, tulianza kwa kuwawa kwanza kujenga jengo la klabu, Mzee Dalali aliona mbali na kununua uwanja Bunju, nasisi tutaanza ujenzi, hii ndio dhima ya uongozi ndani ya Simba kupokezana vijiti vya maendeleo’’.
Kwa upande wake MkurugenziMtendajiwa EAG Group LTD ambao ni washauri watekelezaji wa mikakati ya biashara na masoko wa Simba ImaniKajula alisema ‘’Zoezi la kuteua mabalozi wa Simba ni endelevu na litafika kila kona ya Tanzania. Hawa ni mashabiki ambao mawazo, michango yao ya hali na mali, kutumia ushawishi wao kutaleta maendeleo kwenye klabu yetu. Hawa watakuwa mstari wa mbele kwenye Simba Week kuhamasisha ufanyaji kazi za jamii na kushiriki kwa wapenzi na wapenda maendeleo katika kusukuma maendeleo ya Simba.
Napenda kuwashukuru sana Mabalozi hawa kwa kutenga muda na kuwa tayari kusaidia juhudi za kuiletea Simba maendeleo. Uongozi wangu utakuwa bega kwa bega nanyi katika kazi hii adhimu.
No comments:
Post a Comment