Klabu ya Bayern Munich imesafiri kwa muda wa masaa tisa kutoka Ujerumani hadi China kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa Bundesliga, huo huwa ni utaratibu wa vilabu vingi duniani.
Kizuri zaidi kuhusu safari yao ni mapokezi walioyapata Beijing
mtu wangu zilitumika dakika 30 tu kujaza umati wa watu wasiopungua
1000 kuwapokea huku wakiombwa kusainiwa vitabu vyao vya kumbukumbu
(autographs).
Watu ni wengi wanaohudhuria mazoezi yao,
uwanja ukafurika kama kuna mechi. Mashabiki wamekuwa wakiomba kupiga
picha na wachezaji, lakini pia wachezaji hawakuwa nyuma kuchukua
kumbukumbu zao kwa kupiga picha kwa kutumia simu zao.
Wachezaji kama Philipp Lahm, Manuel Neur na wengine wamekiri kitu kama hicho hutokea mara chache tu.
No comments:
Post a Comment