Pages

July 11, 2015

JOTO LAPANDA DODOMA NEC YAHARISHWA KWA MUDA,MKUTANO MKUU WA CCM KUFANYIKA KESHO

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM)Rais Jakaya Kikwete akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Dodoma leo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Uratibu na Bunge,Jenista Mhagama((shoto)akiteta jambo na Waziri Kiongozi Mstaafu,Shamsi Vuai Nahodha.






Katibu wa Itikadi na Uenezi,Nape Mnauye(kati)akimsikiliza Katibu Mkuu wa Uvccm,Sixbert Mapunda(shoto) na Mnec,Zakhia Meghji.

Waziri Mkuu mstaafu,Edward Lowassa akiwa kwenye kikao cha halmashauri Kuu ya CCM.

Rais Jakaya Kikwete amefungua kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)leo mjini Dodoma  na kuharishwa kwaajili ya mashauriano baada ya baadhi ya wanaCCM kuonesha kutoridhishwa na maamuzi ya Kamati Kuu(CC) ya kuacha jina la Mwanachama waliodhani anakubalika zaidi.

Wakati Mwenyekiti akiingia ukumbini wajumbe walisimama na kuanza kuimba wimbo wa kumusifia Edward Lowassa ambaye jina lake lilikatwa jana usiku na Kamati Kuu.

Baada ya muda mfupi kikao hicho kimeharishwa kwa muda na kutolewa tangazo la Mkutano Mkuu kufanyika kesho jumapili badala ya leo kama ilivyokua imepangwa.

Baadhi ya wajumbe walionekana wakiwa kwenye makundi madogo madogo wakijadiliana la kufanya huku polisi wakiwa kwenye hali ya tahadhari kuimarisha ulinzi makao makuu ya CCM white House.


Jana Kamati Kuu ilipitisha majina matano ambayo ni Bernard Membe,Dk John Magufuli,Dk Asha Rose Migiro,Amina Salum Ally na January Makamba.
Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...