Uchaguzi
umeanza kwenye uwanja wa Nou Camp kumpata Rais mpya wa Barcelona huku
nahodha wa mabingwa hao wa Ulaya Andres Iniesta akiongoza wachezaji wa
zamani na wa sasa kupiga kura kwenye kinyang’anyiro hicho ambacho Josep
Bartomeu anapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi.
Wachezaji
wa zamani na mahodha wa klabu hiyo kwa nyakati tofauti Carles Puyol na
Xavi walikuwa ni miongoni mwa watu waliojitokeza kupiga kura ili kuiweka
klabu yao kwenye mikono salama.
Josep
Bartomeu ni mgombea ambaye anapewa nafasi kubwa ya kuwa rais wa
Barcelona lakini anapata upinzani mkali kutoka Joan Laporta, Austi
Benedito pamoja na Toni Freixa.
Bartomeu
anaonekana kuwa ni chaguo la Luis Enrique (kocha wa Barcelona) baada ya
kupewa mkataba mpya na rais huyo wakati yupo madarakani kabla hajaachia
ngazi kupisha taratibu za uchaguzi ziendelee mwashoni mwa msimu huu.
Laporta
ndiye anaedaiwa kuwa ndiye rais bora kuwahi kutokea kwenye klabu hiyo
kati ya mwaka 2003 hadi 2010 kipindi ambacho Barcelona ilishinda mataji
mawili ya Ulaya (UEFA Champions League).
No comments:
Post a Comment