Mgombea
Ubunge Viti Maalum Vijana Bukoba Bi. Antu Mandoza(Kulia) akirejesha
Fomu ya Kuomba Ridhaa kuteuliwa kugombea Ubunge wa Viti maalum Vijana
Bukoba katika ofisi za umoja huo Mjini Bukoba, ahaidi kuinua Vijana
Kiuchumi endapo atapata nafasi ya kuwa Mbunge wa Vijana.
Mcheza
kwao hutunzwa, Vijana wazidi kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za
Uongozi. Binti Antu Mandoza mwenye kuonekana kuwa na umri miaka 22-25
Amerudisha Fomu za kuwania nafasi ya Ubunge Vijana Viti Maalumu kupitia
CCM. Kwa Mahojiano mafupi ameongelea jinsi anavyopanga kuinua Maisha ya
Vijana kwa kuwatengenezea Fursa na mbinu mbalimbali za kujiajiri pia
kuwaonya kutokukubali kutumika vibaya na MAKUNDI ya Kisiasa
tunapoelekea Uchaguzi kwani ni wajibu wetu Vijana kuilinda Amani yetu.
Mgombea
huyo pia amesema kuwa shauku yake kubwa ni kuwatumikia Vijana kwa
kutatua changamoto ya Ajira na pia ametoa ahadi ya kushirikiana na
Vijana bega kwa bega kuleta maendeleo katika Mkoa wa Kagera.
Binti Antu Mandoza akiweka sawa Kumbukumbu zake katika kitabu mbele ya karani Bi. Jasinta Benedicto wa Umoja wa Vijana Kagera.
Dada Antu Mandoza akiwa kwenye Ofisi za Umoja wa Vijana Bukoba.
Mgombea
Ubunge Viti Maalum Vijana Bukoba Dada Antu Mandoza (kulia) akiptia Fomu
yake ya Kuomba Ridhaa kuteuliwa kugombea Ubunge wa Viti maalum Vijana.
Kushoto ni Bi. Jasinta Benedicto karani wa Umoja wa Vijana Kagera.
Mgombea
Ubunge viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi dada Antu Mandoza
akitoka katika ofisi za umoja wa vijana wa ccm Mkoa wa Kagera baada ya
kuchukua fomu akiwa na Mama yake pamoja na Dada Lilian(kilia nyuma)
إرسال تعليق