Mjumbe
wa Kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu
Lissu, akiongea na wanachama na wananchi kwa ujumla kwenye mkutano wa
kuwatambulisha watia nia ya kugombea nafasi za ubunge na udiwani katika
jimbo la Singida magharibi,mkutano uliofanyika katika Kijiji cha
Puma,tarafa ya Ihanja
Baadhi
ya watia nia ya udiwani na ubunge katika jimbo la Singida magharibi
wakisakata ngoma za asili baada ya kumpokea mgeni rasmi katika mkutano
huo.
Na Jumbe Ismailly,Ikungi
CHAMA
Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Singida kimewaagiza
wanaachama wa chama hicho kuwashughulikia watu wote watakaobainika
kukusanya vitambulisho vya kupigia kura na kuandika namba za
vitambulisho hivyo,kwa lengo la kuihujumu tume,kabla ya kuwafikisha
kwenye vyombo vya sheria.
Mjumbe
wa Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Tundu
Lissu alitoa onyo hilo alipokuwa akiwatambulisha wagombea wa nafasi za
udiwani na ubunge wa jimbo la Singida magharibi,kupitia chama hicho
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Puma,tarafa aya
Ihanja,wilayani Ikungi.
Alifafanua
Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa kambi ya upinzani Bungeni kuwa watu
au mawakala wao wanaotumia nafasi za vyeo vyao kukusanya
vitambulisho,kuandika majina na namba za vitambulisho hivyo,wamekuwa
wakivunja sheria ya uchaguzi kwani wao siyo tume,hivyo watakaobainika
hawana budi kuchukuliwa hatua za kisheria.
“Watu
wanaoandikisha vitambulisho majina na namba hiyo ni kinyume cha sheria
ya uchaguzi wao siyo tume,tunaelewana,wanaandikisha majina ili waje
wavuruge”alisisitiza kiongozi huyo wa kitaifa.
Aidha
Lissu ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Singida mashariki aliweka wazi
kuwa sheria za nchi hata kama watamuuliza askari aliyekuwepo katika
mkutano huo,sheria zinamruhusu raia kukamata mhalifu na endapo mhalifu
huyo anakataa kukamatwa,sheria inaruhusu pia nguvu kiasi itumike.
“Sheria
za nchi hii zinaruhusu raia kukamata mhalifu na kama mhalifu anakataa
kukamatwa,sheria za nchi hii zinaruhusu utumie nguvu kiasi
kumdhibiti,sasa nguvu kiasi na ukiona anataka kukuzidi nguvu ukimpa
kichapo cha uhakika siyo vibaya kabla ya kumfikisha kwenye vyombo vya
sheria”alisisitiza Lissu.
Hata
hivyo mjumbe huyo kamati kuu alihoji sababu za kuandikwa kwa majina ya
watu ili wakayafanyie kitu gani na kuongeza kwamba walijaribu katika
jimbo la Singida mashariki tangu juzi,naye aliwaagiza wawashughulikiea
hadi watakapoamua kuwafikisha polisi wawe wamewalegeza viungo vyao vya
kutosha.
“Hatuwezi
tukafanya mchezo,hatuwezi tukaruhusu uchuro,hatutaruhusu
ujinga,hatutaruhusu uhalifu,sasa kwetu sisi tuna vijiji vyote isipokuwa
vitatu tu,sijui kwenye jimbo la magharibi mna vijiji vingapi,kwani
anayekamatwa mpaka atakapofikishwa polisi anakuwa amelowa vya
kutosha”alibainisha kwa msisitizo.
Kwa
upande wake mbunge wa viti maalumu aliyemaliza muda wake,Christowaja
Mtinda akijitambulisha kwa wanachama alisisitiza kwamba akina mama
wajawazito,watoto wenye umri chini ya miaka mitano,wazee na walemavu
wanatakiwa kupatiwa huduma za afya bure.
No comments:
Post a Comment