Pages

July 25, 2015

BARRACK OBAMA AWASILI NCHINI KENYA

Rais wa Marekani, Barack Obama akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta. Pamoja nae ni Mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta. Obama aliwasili nandege yake ya Air Force One.
Rais wa Marekani, Barack Obama akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta. Pamoja nae ni Mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.
Mtoto Joan Wamaitha, 8, ndiye Mkenya wa kwanza kumkaribisha Rais Barrack Obama nchini humo kwa kumpa shada la maua na kupiganae picha kadhaa za kumbukumbu kabla ya kwenda kulakiwa na mwenyejiwake Rais Uhuru Kenyatta.
 Rais wa Marekani, Barack Obama akisalimiana na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta . 
Rais wa Marekani, Barack Obama akikumbatiana na dada yake Auma Obama huku Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akiwaangalia.
 **************
Ndege iliyombeba rais obama ilitua katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta muda mfupi baada ya saa mbili za usiku.

Alipowasili Rais Obama amelakiwa na mweyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.
mwendo wa saa mbili na robo rais Obama alitua ndege yake.

Alipowasili alizungumza kwa muda mfupi na mwenyeji wake Rais Kenyatta na kisha kutia saini kitabu cha wageni kabla ya kuondoka.

Obama sasa ameandikisha historia ya kuwa Rais wa kwanza wa Marekani, kuzuru Kenya akiwa ofisini.

Obama anatarajiwa kufungua mkutano wa sita wa kimataifa kuhusu ujasiria mali katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi.

Baadaye rais huyo atafanya mashauriano na Rais Uhuru Kenyatta, Ikulu ya Nairobi.

Siku ya Jumapili rais Obama atahutubia mkutano wa wakuu wa mashirika ya kijamii katika chuo kikuu cha Kenyatta kabla ya kuhutubia mkutano mwingine kwa wakenya wote katika uwanja wa Kasarani.

Obama anatarajiwa kuondoka siku ya Jumapili kuelekea nchini Ethiopia. Source:BBC Swahili & AFP

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...