Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, (NEC),
Beng’ Issa, (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Benjki ya Posta, Sabasaba
Moshingi, (wapilia kulia), Rais wa VICOBA Endelevu Tanzania, Devota
Likokola, (wapili kushoto), Mwanasheria wa Benki ya Posta Tanzania,
Mystica Mapunda Ngongi, (wakwanza kulia), wakiwa wameshikana mikono
baada ya benki hiyo kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano kati ya
baraza na benki hiyo, katika kuwawezwesha wana VICOBA kiuchumi. Hafla
hiyo ilifanyika leo Julai 14, 2015. kwenye ukumbi wa wizara ya fedha
jijin I Dar es Salaam.
BARAZA
la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, (NDC), na Benki ya Posta
Tanzania, (TPB), wamesaini makubaliano ya ushirikiano wa kuwawezesha
wanachama wa VCOBA nchini.
Akizungumza
wakati wa hafla ya kutiliana saini makubaliano nhayo kwenye ukumbi wa
wizara ya fedha jijini Dar es Salaam leo Julai 14, 2015, Katib u
Mtendaji wa baraza hilo, Beng’ Issa, alisema, Katika juhudi za
kuwawezesha watanzania kiuchumi kupitia upatikanaji wa mitaji na
kuendeleza ujasirimali nchini, Serikali kupitia Sheria ya Taifa ya
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004, ibara ya IV, sehemu ya 16
iliagiza uanzishwaji wa Mfuko wa Taifa wa Uwezeshaji Mwanachi yaani
‘’Mwananchi Empowerment Fund,”.
“Katika
kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa mitaji yenye gharama nafuu kwa
wajasiriamali nchini, Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
limesaini hati za makubaliano na Benki ya Posta Tanzania katika
kusimamia udhamini wa mikopo yenye masharti nafuu kwa makundi mbali
mbali ya wajasiriamali nchini yanayokidhi masharti husika.” Alisema
Beng’i.
Mfuko
huu utakao simamiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
ni pamoja na kutoa fursa kwa wananchi katika makundi au mtu mmoja mmoja
kupata mitaji ya kuwekeza kwenye miradi ya kiuchumi kupitia mikopo ya
moja kwa moja au udhamini (direct lending or guarantee system).
Ili
kutimiza azama hiyo baraza limeamua kushirikiana na benki ya ;posta
Tanzania ambayo ina mtandao mpana, kutekeleza azma hiyo ambapo
wananchama wa VICOBA, watapata mikopo na mafunzo kutoka benki ya posata.
Kwa
aupande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi,
alisema, benki yake ni benki ya wananchi na hivyo unayo furaha kubwa
kushirikiana na NE, ili kuwakwamua wananchi kiuchumi kwa kupata mikopo
itakayowazsaidia kuendesha shughuli zao za kiuchumi.
“Benki
ya Posta inayo furaha kubwa kushirikiana na Baraza hili ili kuwawezesha
wananchi wengi zaidi kupata huduma za kifedha kwa gharama nafuu kupitia
mpango huu.” Alifafanua Moshingi.
Alisema,
Benki ya Posta inaamini kuwa hii ni fursa muhimu kwa vikundi hivi
visivyo rasmi kufungua akaunti na kuweka fedha zao mahala salama. Hili
litawawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi zaidi, na hatimaye
wataweza kupatiwa mikopo nafuu kwa ajili ya kukuza biashara zao. Hadi
sasa Benki imefungua zaidi ya akaunti 340 za vikundi. Vikundi hivi
vitafaidika pia na huduma ya TPB POPOTE, itakayo wawezesha kupata huduma
za kifedha popote pale walipo.
No comments:
Post a Comment