Pages

July 17, 2015

BANZA STONE AFARIKI DUNIA, KUZIKWA KESHO MAKABURI YA SINZA DAR ES SALAAM

Mwanamuziki wa muziki wa dansi aliyepata kushika chati za juu katika utunzi na uimbaji katika bendi mbalimbali nchini za muziki wa Dansi, Ramadhani Masanja 'Banza Stone' amefariki dunia hii leo m,chana nyumbani kwao Sinza Kijiweni Dar es Salaam.

Kwa Mujibu wa Mmoja wa wanafamilia ya Marehemu, Banza anataraji kuzikwa kesho saa 10 jioni katika makaburi ya Sinza.

Aidha Mwanafamilia huyo amesema Mwili wa marehemu kabla ya mazishi utaswaliwa Lion uliopo Sinza Dar es Salaam. 

Banza Stone atakubwa na wengi hasa kutiokana na nyimbo zake nyingi ambazo ziliweza kuwabadili watanzania na hulka ya kuwapenda wanamuziki wa nje hasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 

Banza stone alijizolea umaarufu mkubwa wakati alipojiunga na kuanzisha bendi ya Afrika Stars 'Twanga Pepeta' iliyo tamba na kiionjo cha Kisima cha Burudani Eeeebaba!! 

Katika sanaa hiyo ya muziki Banza alianza harakati za muziki miaka ya 1990 wakati huo akisoma elimu ya dini ya Kiislamu katika madrasaBanza aliwahi kufanyakazi na bendi ya Twanga Pepeta, African Stars, TOT, Bambino na Extra Bongo .

Mionongoni mwa nyimbo ambazo banza atakumbukwa nazo ni Mtu Pesa, Sisi ndo Sisi, Mtaji wa Masikini, Utanikumbuka, na ile inayotumiwa sana na wapenzi wa Simba, Angurumapo Simba Mcheza Nani.

Nyimbo hizo aliimba na wasanii mbalimbali aliokuwa akifanya nao kazi kama Ali Choki, Luiza Mbutu, Super Ngedere na wengineo wengi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...