Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Vangimembe Lukuvi
akikata utepe kuzindua ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na
NHC Mjini Kahama. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw.
Felix Maagi
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe
Lukuvi(aliyevaa miwani) akiweka jiwe la msingi katika nyumba
zilizojengwa na NHC Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Hizi
ni miongoni mwa nyumba 50 za gharama nafuu zilizojengwa na NHC katika
mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula katika halmashauri ya Mji Kahama
mkoani Shinyanga. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini
Mh.William Vangimembe Lukuvi ameweka jiwe la msingi katika nyumba hizo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC Bw. Haikamen Mlekio akitoa
maelezo kwa Waziri Lukuvi kuhusu hatua zilizofikiwa katika mradi wa
nyumba 50 zinazojengwa na NHC Wilayani Kahama ulioanza kujengwa mwezi
Januari mwaka 2015 na kutarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2015.
Waziri
Lukuvi akitizama michoro ya mradi wa nyumba 50 utakaogharimu kiasi cha
shilingi bilioni 2.1 unaotekelezwa na NHC Wilayani Kahama.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akikagua
majengo ya nyumba 50 zinazojengwa na NHC eneo la Bukondamoyo Wilayani
Kahama akiambatana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Felix Maagi
(kushoto)
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Mh.William Vangimembe
Lukuvi akiwasili kuweka jiwe la msingi zilizojengwa na NHC eneo la
Bukondamoyo Mjini Kahama.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi
akielekea kwenye ya mfano ili kuikagua na kukata utepe kuashiria
uzinduzi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Mjini
Kahama.
Wa
pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Felix Maagi akitoa
maelezo kwa Waziri Lukuvi baada ya kukagua moja ya majengo hayo 50
yaliyojengwa na NHC eneo la Bukondamoyo Wilayani Kahama.
Meza Kuu- Waziri Lukuvi akitazama kikundi cha ngoma wakati alizindua nyumba za gharama nafuu za NHC Mjini Kahama lengo
likiwa la kupendezesha mandhari ya miji yetu, kupandisha hadhi ya
maeneo lakini pia kuwapatia wananchi wa kipato cha chini nyumba bora na
gharama nafuu
Kundi la sanaa la Makhirikhiri la Kahama wakitoa burudani
Mkuu
wa Wilaya ya Kahama Bw. Benson Mpesya akizungumza eneo la Bukondamoyo
na kulipongeza Shirika la Nyumba la Taifa kwa kujenga nyumba za kisasa
na imara na kutoa msaada wa mashine za kufyatulia matofali katika
halmashauri za wilaya nchini.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa NHC,, Bw. Felix Maagi akizungumza eneo la
Bukondamoyo ambapo alisema halmashauri zitakazotoa ushirikiano na kuwa
tayari kununua nyumba ndizo zitazojengewa nyumba na NHC. Bw. Felix Maagi, alisema pia kuwa mradi huo umetengeza ajira za moja kwa moja 290, ajira shirikishi 145 na makazi ya watu 300.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini William Lukuvi
akiwahutubia wakazi wa Kahama katika eneo la mradi wa nyumba 50
zilizojengwa na NHC katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula Wilayani
Kahama. Alizitaka
Halmashauri za Wilaya kupima maeneo ya Miji na kuyagawa kwa wananchi
kwa utaratibu unaotakiwa ili kuondoa migogoro ya ardhi na kuweka mipango
miji vizuri.
Mbunge
wa Jimbo la Kahama Mh. James Lembeli akizungumza katika eneo la mradi
ambapo aliwataka wakazi wa Kahama kuchangamkia fursa ya nyumba hizo kwa
kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ya kibiashara katika eneo hilo ili
fedha za watu watakaoishi hapo zisitoke nje ya eneo hilo.
Waziri
William Vangimembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali
wealiohudhuria uzinduzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC
eneo la Bukondamoyo Mjini Kahama.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Mh. William Lukuvi akiondoka
eneo la tukio akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Felix Maagi
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi
akiagana na Mbunge wa Jimbo la Kahama Mh. James Daudi Lembeli mara baada
ya kuzindua nyumba za gharama nafuu eneo la Bukondamoyo.
No comments:
Post a Comment