Ofisa
Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,
Benjamin Majoya akikata utepe kuzindua rasmi kisima cha maji
kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa gharama
ya sh. mil 56, katika Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang'anda,
Mkuranga, Mkoa wa Pwani. Kushoto ni Diwani wa Kata hiyo, Karu Karavina na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo (wa pili kulia).
Ofisa
Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,
Benjamin Majoya (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto kwake) pamoja na
Diwani wa Kata ya Kiparang'anda, Karu Karavina (kushoto) wakifurahi
baada kukabidhi mradi wa kisima cha maji kwa wananchi wa Kijiji cha
Magoza, wilayani Mkuranga mwishoni mwa wiki. Kisima hicho kimejengwa kwa
msaada wa TBL gharama ya sh. mil. 56.
Akina mama wakicheza kwa furaha wakati wa hafla ya kukabidhiwa kisima chas maji na TBL
Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu akitoa utambulisho wakati wa hafla hiyo
Ofisa
Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,
Benjamin Majoya akimtwisha ndoo ya maji Mama mkazi wa Kijiji cha
Magoza, Kata ya Kiparang'anda, wilayani Mkuranga, Pwani, wakati wa hafla
ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kukabidhi msaada wa kisima cha maji
kilichojengwa kwa gharama ya sh. mil. 56 kijijini hapo. Makabidhiano
hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki.
Mmoja wa akina mama akifurahia baada ya kuteka maji kwenye kisima hicho
Mkurugenzi
wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo akielezea mikakati ya
kuisaidia jamii katika uboreshaji wa sekta ya maji nchini kutoka sehemu
na faida inayopatikana katika mauzo ya vinywaji vyao
Diwani wa Kata ya Kiparang'anda, akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwapatia msaada huo wa kisima.
Wakifunua pazia kuzindua mradi huo wa kisima
Mgeni rasmi, Benjamin Majoya akifungua maji ya bomba badaa ya kuzindua kisima hicho
Steve Kilindo wa TBL, akinywa maji baada ya kuzindua kisima hicho
No comments:
Post a Comment