Pages

June 15, 2015

LOWASSA APATA UDHAMINI WA KISHINDO KATIKA MIKOA YA KATAVI LA RUKWA JANA.

 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Mselem Said Abdallah (shati la kitenge) akizungumza machache wakati wa kumkaribisha, Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa, wakati alipofika kwenye ofisi za Chama hicho, Mpanda, Mkoani Katavi  Juni 14, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
 Baadhi ya wananchi wa Mji wa Mpanda wakionekana ni wenye furaha nyingi pindi walipomuona Mh. Edward Lowassa akipita kwenye maeneo yao wakati akielekea Ofisi za CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoani Katavi  Juni 14, 2015.
 Mapokezi ya Mh. Lowassa mjini Mpanda, Katavi .
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa akiwapungia wananchi wa mji wa Mpanda, Mkoani Katavi waliojitokeza kumlaki, wakati alipofika kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoani Katavi, alikofika Juni 14, 2015 kwa ajili ya kutafuta udhamini wa wanaCCM ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. alie mbele yake ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Mselem Said Abdallah.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Mselem Said Abdallah akimuongoza Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa kuingia kwenye Ukumbi wa CCM wilaya ya Mpanda, Mkoani Katavi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Mselem Said Abdallah.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu zenye majina ya wanaCCM wa Mkoa wa Katavi  Juni 14, 2015, waliomdhani ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Anaekabidhi fomu hizo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda, Bi. Elizabert Kashira. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 3440 mkoani Katavi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Mselem Said Abdallah akizungumza machache mara baada ya Mh. Lowassa (pili kulia) kukabidhiwa fomu za wadhamini wa CCM za kumuwezesha kutata ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Wengine pichani toka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mngeja, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Dkt. Aman Kaburou pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpanda, Beda Katani.

Wana Mpanda haoo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Mselem Said Abdallah akimkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa ili aweze kuwashukuru wanaCCM wa Mpanda kwa kumdhani ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkomo maelfu ya wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Mpanda, waliofurika kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoani Katavi  Juni 14, 2015.Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 3440 mkoani Katavi. 
Umati wa watu nje ya Ofisi za CCM Mpanda.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Rukwa,  Juni 14, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono wanaCCM na wananchi wa Mji wa Sumbawanga, Mkoani Rukwa  Juni 14, 2015.

Mjumbe wa NEC ya CCM kutoka Mlele, Bw. Kampala akiwasalimia wanaCCM wa mji wa Sumbawanga.
"Salaam wanaCCM wenzangu.


Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na wanaCCM wa Mji wa Sumbawanga, Mkoani Rukwa wakati alipofika kutafuta udhamini wa kupewa ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Jumla ya wanCCM 4045 wamemdhamini.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...