Na Mwandishi Maalum, New York
Umoja wa Mataifa wiki hii, umekamilisha mikutano muhimu miwili kati ya mingi, ambapo ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioshiriki majadiliano ya mikutano hiyo waliiwakilisha vema nchi yao.
Moja ya mikutano hiyo ni ule wa marejeo ya Mkataba wa kuzuia usambaaji na uzalishaji wa silaha za nyukilia, matumizi yake, ikiwa ni pamoja na silaha nyingine za maangamizi ( NPT), Mkutano huu ambao umefanyika kwa mwezi mzima, ukitawaliwa na majadiliano makali juu ya mada mbalimbali muhimu zinazohusiana na marejeo ya mkataba huo. Bado hadi siku ya mwisho ya mkutano ( Ijumaa) wajumbe wamemaliza mkutano pasi kufikia makubaliano ya pamoja ya vipengele kadhaa vya tamko la mwisho la mkutano.
Katika kile kilichooneka wazi kwamba wajumbe wamekubali kuto kukubaliana, ni kwa baadhi ya mataifa hasa yale ya magharibi na yenye silaha za nyukilia kutoonyesha utayari na utashi wa kisiasa wa kuungano mkono baadhi ya mambo kadhaa likiwamo la kufanyika kwa mkutano wa Ukanda Huru usio na silaha za Nyukilia katika Eneo la Mashariki ya Kati .
Mataifa kama vile Marekani, Uingereza na Canada yalisimamia kidete misimamo yao ya kupinga kuingizwa katika tamko la mwisho la mkutano wa NPT sehemu inayopendekezwa kufanyika kwa mkutano huo huko Mashariki ya Kati, kwa kile walichodai kwamba baadhi ya mataifa yamelipenyeza suala hilo bila ya ushirikishwaji wa nchi nyingine ikiwa Israel jambo ambalo wamesema hawakubaliani nalo.
Mkutano kuhusu ukanda huru usio wa silaha za nyukilia katika eneo la Mashariki ya Kati, umeshindikana kufanyia kwa muda mrefu sasa licha ya maazimio mbalimbali yanatoaka ufanyika.
Kushindwa kwa mkutano huo ambao unaelekezwa kama muhimu kwa mustakabali wa hali ya amani na usalama katika eneohilo, unatokana kwa kiasi kikubwa kukosekana kwa uungwaji mmono usio na shaka kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwamo Israeli ambayo imekuwa ikilalamikwa na baadhi ya mataifa ya Kiaarabu.
Israel si mwanchama wa NPT. lakini pia inasadikiwa inamiliki silaha za nyukilia ingawa haijatamka hadharani. Mataifa mengi yakiwamo yakiiarabu yamekuwa yakilitaka taifa hilo kutamka mbele ya Jumuiya ya Kimataifa kwamba inamiliki silaha hizo lakini imekuwa ikikingiwa kifua na baadhi ya mataifa makubwa.
Eneo jingine ambalo wajumbe wameshindwa kukubaliana kwa kauli moja ni pendekezo la kuingizia kwenye mkataba huo sehemu itakayozungumzia madhara ya kibinadamu yatakayo na matumizi ya silaha za nyukilia. Eneo hili nalo limezua mjadala mzito kiasi kwamba licha ya umuhimu wake kwa uhai wa mwanadamua na viumbe hai likashindwa pia kufikia makubaliano ya pamoja.
Rasmu ya tamko la mwisho la mkutano huo limepitishwa kwa vifungu kutokana na kile ambacho wajumbe wamesema ni kutoridhishwa kwa maudhui mazima ya tamko hilo huku wengine wakieleza kwamba, baadhi ya vifungu ambayo vilipitishwa kwa makubaliano wakati wa majadiliano ya wiki nne havikuingizwa katika tamko hilo
Wazungumzaji wengi katika siku ya mwisho ya mkutano huu ambao ulikwenda hadi saa tatu usiku, siku ya ijumaa, wameelezea masikitiko yao ya kukosekana kwa fursa ya kusukuma mbele utekelezaji wa NPT kwa sababu tu ya baadhi ya nchi kusimamia maslahi binafsi badala ya maslahi ya jumla.
Mkutano wa pili ambao nao ulikuwa na mvutano wa aina yake ni ule uliokuwa ukijadili maandalizi ya ajenda na malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya 2015 ( SDGs). Mkutano huu wa wiki moja na ambao pia ulimalizika siku ya ijumaa, wajumbe licha ya kukubaliana na maudhui mazima ya haja na umuhimu wa kufanyika kwa tathmini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa SDGs, wajumbe walishindwa kukubaliana kwa kauli moja mada au ajenda zitakazo jadiliwa wakati wa mkutano wa Kisiasa wa Ngazi ya Juu wa viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali utakaofanyika mwezi Septemba 2015
Mkutano huo wa Kilele wa Kisiasa wa viongozi unatarajiwa kupokea na kupitisha ajenda na malengo ya maendeleo endelevu baada ya 2015, mkutano ambao pia utakuwa na miduara ya majadiliano ya maada mbalimbali.
Katika maandalizi ya mkutano huo, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa aliziomba nchi wanachama kuunda mada zikazojadiliwa katika mkutano huo, maanda mabazo kimaudhui zinatakiwa kwenda na SDGs.
Kwa wiki kadhaa nchi wanachama kupitia makundi yao ya kikanda walikuwa na kazi kubwa ya kubuni mada hizo, kuzijadilia na kisha kukubaliana zile ambazo wanaamini ndizo muhimu.
Mada ambazo zimependekezwa ni pamoja na mada itakayojadili kumaliza umaskini na tatizo la njaa, kukabiliana na ukosefu wa usawa, uwezeshwaji wa wanawake na wasichana bila kuacha mtu nyuma, kukuza uchumi endelevu na kuleta mabadiliko katika uzalishaji na kiwango cha matumizi na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ili kuilinda dunia.
Mada nyingine zinazopendekezwa ni kujenga ufanisi, uwajibikaji ili kufikia maendeleo endelevu, kukuza ushirikiano wa kimataifa, kujenga misingi imara ya uwajibikaji na taasisi jumuishi ili kufikia maendeleo endelevu na kukuza ushirikiano wa kimataifa.
Pamoja na kukuballiana juu ya mada hizo, washiriki wa mkutano huu walishindwa kukubaliana juu ya maudhui pana iliyoainisha kila mada. Kutokana nakwamba kila nchi au kundi wakilishi lilikuwa na tafsiri tofauti ya maelezo ya ziada ya mada hizo.
Matokeo ya kushindwa kukubaliana kuhusu maudhui pana au maelezo yakina ya baadhi mada na baada ya majadiliano ya kujaribu kupata muafaka kati ya pande zinazopinga kushindwa kuafikiana, Wenyeviti- wenza wa majadiliano hayo walieleza kwamba kutokana na wajumbe kutokubaliana basi mada hizo zitapelekwa kwa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa maamuzi.
Ilikubaliwa katika mkutano huo kwamba mada hizo ziwasiliwe kwa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, bila ya maelezo ya ziada kuhusiana na mada zenyewe kwa vile nchi wanachama zilishindwa kukubaliana.
No comments:
Post a Comment