Pages

May 25, 2015

TAASISI YA PAN AFRICAN LAWYERS UNION(PALU) NA MAHAKAMA YA AFRIKA YATAMBUA UMUHIMU WA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu(AfCPHR)yenye makao yake jijini Arusha,Jaji  Mstaafu wa Tanzania,Augustino Ramadhani(katikati)akizungumza katika hafla ya chakula cha jioni kilichondaliwa na taasisi ya Pan African Lawyers  Union(PALU)kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa PALU,Donald Deya na kulia ni Mkuu wa mawasiliano wa AfCPHR,Sukhdev Chatbar.Alisisitiza umuhimu wa nchi zaidi za Afrika kutoa tamko la kuitambua Mahakama hiyo ili kutoa fursa kwa watu binafsi na asasi za kiraia kuitumia ipasavyo mahakama hiyo.

Waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki wakisikiliza hotuba fupi ya Jaji Augustino Ramadhani.

Baadhi ya maafisa wa AfCPHR,PALU na waandishi wa habari wakifatilia hafla hiyo.

Mwandishi wa habari wa siku nyingi ambaye alikua mwezeshaji Mkuu katika mafunzo ya waandishi wa habari ,Jenerali Ulimwengu(kushoto)akiwa amejumuika na waandishi wa habari.

Waandishi wa habari wakifurahia moja ya picha ya tukio la hafla ya chakula cha jioni kwenye ofisi za PALU.

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu(AfCPHR)yenye makao yake jijini Arusha,Jaji  Mstaafu wa Tanzania,Augustino Ramadhani(Kulia)akimkabidhi cheti cha kushiriki mafunzo ya namna Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu inavyofanya kazi zake mwandishi wa habari wa IPP,Asraji Mvungi.

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu(AfCPHR)yenye makao yake jijini Arusha,Jaji  Mstaafu wa Tanzania,Augustino Ramadhani(Kulia)akimkabidhi cheti cha kushiriki mafunzo ya namna Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu inavyofanya kazi zake mwandishi wa habari wa gazeti la New Vision nchini Uganda,Mosses Warugembe.
Habari picha na www.rweyemamuinfo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...