Walimu kutoka sehemu mbalimbali nchini wakiwa katika mkutano wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) unaondelea jijini Arusha wakifuatilia kwa makini mada za mkutano huo .Picha na Ferdinand Shayo |
Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete akisalimiana na walimu waliofika katika mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) unaoendelea jijini Arusha . |
Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete akisalimiana na walimu waliofika katika mkutano wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) |
Walimu kutoka sehemu mbali mbali nchini waliohudhuria katika mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) |
Na Ferdinand
Shayo,Arusha.
Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa walimu watarajie nyongeza
ya mishahara itakayoanza mwezi Agosti mwaka huu ikiwa ni moja kati ya jitihada
za serikali katika kuboresha maslahi ya walimu nchini.
Kikwete akihutubia Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania
(CWT ) uliofanyika jijini Arusha amesema kuwa nyongeza hiyo itahusisha
walimu wote wanaolipwa kima cha chini
cha mshahara na kima cha juu pasipo kutaja kiwango kilichoongezeka.
“Wakati mnachukua mishahara yenu benki mwezi Agosti mtaona
tofauti ambayo ni nyongeza ya mshahara ,wenzenu wa chama cha Wafanyakazi
waliniomba nisitangaze niongeze kimya
kimya ili wafanyabiashara wasipandishe bei ya bidhaa” alisema Rais Kikwete
Aidha Rais Kikwete amesema kuwa serikali inaendelea na
jitihada za kuhakikisha kuwa inaboresha elimu nchini ikiwa ni pamoja na kuboresha
maslahi ya walimu nchini,kuongeza vifaa vya kujifunzia na kufundishia,nyumba za
walimu,vitabu na maabara.
Amesema kuwa madai ya walimu wanayoidai serikali yatalipwa
kwa awamu iwapo uhakiki utakamilika kwa sasa wanatarajia kulipa kiasi cha
shilingi bilioni 7 kwa walimu 70100 watalipwa Agosti mwaka huu.
“Katika kufanya uhakiki wa madai ya walimu ikiwemo
malimbikizo ya mishahara,posho za kufundishia,uhamisho tuligundua kuwa wako
baadhi ya watu walifanya udanganyifu lakini sasa tunamalizia kufanya uhakiki
ili fedha hizo zilipwe” Alisema Kikwete
Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Alhaji Yahaya
Msulya amemtaka Rais Kikwete kushughulikia suala la posho ya kufundishia kwa
walimu kwani walimu ni kundi linalofanya kazi kwa muda mrefu kuliko watumishi
wengine wa serikali.
“Mwalimu anaingia shuleni saa 1:30 asubuhi anatoka saa 3:00
mda huo anatakiwa kusahihisha kazi za wanafunzi na kuandaa masomo ya kufundisha
kesho hivyo anatumia muda mwingi sana katika kazi ni vyema serikali
ikaliangalia suala hili” alisema Msulya
Katibu huyo ameupongeza uamuzi wa serikali kutoa bure elimu
ya msingi na sekondari ambao utawasaidia watoto wengi hasa waliotoka kwenye
familia zenye kipato cha chini.
No comments:
Post a Comment