Waziri
mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa
akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu
katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya
kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee
hiyo(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Waziri
mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowasa akiwa sheikh
mkuu wa Bakwata mkoani Arusha,Shaaban Juma wakifurahia jambo katika
hafla ya harambe ya ujenzi wa msikiti wa Patandi iliyofanyika jana
katika uwanja wa msikiti mkuu wa mkoa Arusha,jumla ya kiasi cha zaidi ya
sh,200 milioni zilipatikana.
Waziri
mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa
akiwa anasalimiana na baadhi ya wadau waliokuja kumuunga mkono katika
uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa
Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana
katika harambee
Msafara wa pikipiki
Waziri
mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa
anatarajia kutangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais kupitia CCM mnamo
Mei 24 mwaka huu katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid uliopo
jijini Arusha.
Lowasa,alitoa
kauli hiyo leo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa
Patandi ambapo alifanikisha kuchangisha jumla ya zaidi ya kiasi cha
sh,200 milioni ambapo watu mbalimbali walimuunga mkono katika harambee
hiyo.
Akizungumza
katika hafla hiyo leo kwa mafumbo Lowasa alisema kuwa mnamo Mei 24
mwaka huu anataraji kusema neno ambalo atahitaji wananchi wamuunge mkono
siku hiyo.
"Niseme
neno nisiseme,tarehe 24 mwezi huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid
siku hiyo nitasema neno ambalo nitahitaji mniunge mkono ambalo
nitahitaji mniunge mkono "alisema Lowasa
Lowasa
kwa kujiamini aliwaomba kila mkazi wa Arusha siku hiyo kutoka na kuja
uwanja huo na kumuunga mkono katika safari yake ya matumaini.
"Ukiulizwa unaenda wapi sema unakuja kuniunga mkono katika safari yangu ya matumaini"alisisitiza Lowasa
Hatahivyo,Lowasa
aliipongeza kamati ya amani ya mkoa wa Arusha inayoundwa chini ya
Askofu wa kanisa katoliki la jimbo kuu mkoani Arusha,Josephat lobullu
kusimamia amani ya mkoa huo.
Aliipongeza
kamati hiyo na kusema kuwa amani ya mkoa wa Arusha ni muhimu kuliko
jambo lolote kwa kuwa Arusha ni mji ambo ni chanzo cha utalii duniani.
"Tuendelee
kuheshimiana bila kujali misingi ya dini,kabila au rangi lakini
niipongeze kamati ya amani ya hapa Arusha kwa kuwa Arusha ni mji wa
kitalii bila amani hakuna utalii Arusha"alisema Lowasa na kuibua shangwe.
Chanzo:Michuziblog

Post a Comment