KAMPUNI YA UJENZI YA CHINA YAJENGA MADARASA MAWILI MURIET ARUSHA


Balozi wa China hapa nchini,Dk Lu Youqing akisalimiana na wanafunzi wa darasa la kwanza wa Shule mpya ya Msingi Murieti,Kata ya Sokon 1 jiji la Arusha  wakati akiwasili kukabidhi madarasa mawili yaliyojengwa kwa msaada na kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering Corporation Africa Ltd,wengine ni Naibu Meya wa jiji la Arusha,Prosper Msofe(katikati)na Mkuu wa wilaya ya Arusha,Christopher Kangoye.

Balozi wa China hapa nchini,Lu Youqing akigawa zawadi za mabegi na mipira ya miguu na Pete kwa wanafunzi wa darasa la kwanza wa Shule mpya ya Msingi Murieti,Kata ya Sokon 1 jiji la Arusha  wakati wa kukabidhi madarasa mawili yaliyojengwa kwa msaada na kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering Corporation Africa Ltd.Picha na Filbert Rweyemamu     

Arusha.Balozi wa China nchini Tanzania, Dk. Lu Youqing,amesema serikali yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo ya elimu kama njia mojawapo ya kupiga vita umasikini.
 
Alisema hayo  jijini Arusha wakati akikabidhi madarasa mawili katika Shule mpya ya Msingi ya Muriet iliyopo Kata ya Sokon 1 yaliyojengwa kwa msaada na kampuni ya ujenzi ya Jiangxi Geo-Egineering(Group)Corporation.
 
“Uwepo wa Shule hii ni ukombozi  mkubwa kwa watoto hawa ambao hawalazimiki kutembea umbali mrefu kwaajili ya kutafuta elimu ambayo ni msingi wa maendeleo ya kila mtu na nyenzo ya kupambana na umasikini,”alisema Dk Lu
 
Hata hivyo aliishauri serikali kuongeza walimu idadi ya walimu kutoka wanane waliopo ukilinganisha na idadi ya wanafunzi 350 walioandikishwa darasa la kwanza mwaka huu.
 
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Christopher Kangoye alisema kampuni hiyo imeonesha uungwana wa kuchangia miradi ya maendeleo baada ya kuona mahitaji wakati ikijenga miundombinu ya jiji na kuliweka Jalala Kuu katika hali ya kisasa ambayo haithiri afya za wananchi wanaozunguka eneo hilo.
 
“Ningependa makampuni mengine yaige mfano ulioneshwa na Jiangxi Geo-Engineering kwa kutoa sehemu ya faida waliyoipata kuirejesha kwa jamii ili inufaike na kama jamii zingine,elimu ni  msingi wa maendeleo yetu,”alisema Kangoye
 
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa  kampuni hiyo,Ye Chengbiao alisema wametumia kiasi cha Sh 25 milioni kukamilisha ujenzi huo na kuweka meza na viti vya kisasa baada ya kupata ushirikiano wa serikali ya halmashauri ya Jiji na wananchi wa Muriet.

Post a Comment

Previous Post Next Post