HALI ILIVYOKUA KATIKA CHUO KIKUU CHA GARRISA NCHINI KENYA JANA

Ramani ya chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya
Takriban watu 15 wanaodaiwa kufunika nyuso zao wameshambulia chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini Mashariki mwa Kenya.
Watu hao wanaodaiwa kuingia katika taasisi hiyo mwendo wa saa kumi asubuhi wakati ambapo waislamu walikuwa wakifanya sala yao ya alfajiri.
Hata hivyo maafisa wa polisi wanasema kuwa shambulizi hilo lilifanyika mwendo wa saa kumi na moja unusu.
wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa
Mwandishi wa BBC mjini humo anasema kuwa walinzi wawili waliuawa katika lango la chuo hicho huku maafisa wawili wa polisi waliokuwa wakilinda chuo hicho pamoja na wanafunzi wakijeruhiwa.
Walioshuhudia wanasema kuwa kumekuwa na majeruhi mengi ndani ya chuo hicho.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho waliosalimika
Jeshi la Kenya KDF ,maafisa wa polisi na ambulansi walifika katika eneo la tukio na sasa wameingia ndani ya majengo ya chuo hicho ambapo kumekuwa na ufyatulianaji wa risasi kati ya washambuliaji na maafisa wa jeshi.
Waislamu na wakristo waliotekwa ndani ya Jumba hilo la Chuo kikuu cha garissa wamedaiwa kutawanywa kabla ya waislamu 15 kuwachiliwa huru kulingana na msemaji wa kundi hilo la Alshabaab.
Maafisa wa Polisi wa Kenya
kundi la wapiganaji wa Alshabaab limesema kuwa liko ndani ya Chuo hicho kikuu na limewatawanya waislamu na wakristo
Wapiganaji wamedaiwa kuwateka nyara wanafunzi na kuwaua watu 147 katika chuo hicho kulingana na wafanyakazi wa msaada na maafisa wa polisi.Takriban watu 65 wengine wamejeruhiwa baada ya washambuliaji kuvamia chuo hicho.

Alshabaab lakiri kutekeleza shambulizi
Kundi la wapiganaji wa Al-shabaab limekiri kutekeleza shambulizi katika chuo kikuu cha Garissa Kaskazini Mashariki mwa Kenya.
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya

Baadhi ya wanafunzi wamedaiwa kutoroka kutoka mabweni waliokuwa wakilala
Wapiganaji hao wanaodaiwa kuwa watano wanaaminika kuwa ndani ya jengo hilo la Chuo kikuu .
Maafisa wa polisi wakikabiliana na wapiganaji huko Garissa Kenya
Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya linasema kuwa watu 30 wamejeruhiwa huku wanne kati yao wakiwa na majeraha mabaya..Kwa sasa shirika hilo linawasafirisha madaktari katika eneo hilo.
 .BBC Swahili

Post a Comment

Previous Post Next Post