Ramani ya chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya
Takriban watu 15 wanaodaiwa kufunika nyuso zao wameshambulia chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini Mashariki mwa Kenya.
Watu
hao wanaodaiwa kuingia katika taasisi hiyo mwendo wa saa kumi asubuhi
wakati ambapo waislamu walikuwa wakifanya sala yao ya alfajiri.
Hata hivyo maafisa wa polisi wanasema kuwa shambulizi hilo lilifanyika mwendo wa saa kumi na moja unusu.

Mwandishi
wa BBC mjini humo anasema kuwa walinzi wawili waliuawa katika lango la
chuo hicho huku maafisa wawili wa polisi waliokuwa wakilinda chuo hicho
pamoja na wanafunzi wakijeruhiwa.
Walioshuhudia wanasema kuwa kumekuwa na majeruhi mengi ndani ya chuo hicho.

Jeshi
la Kenya KDF ,maafisa wa polisi na ambulansi walifika katika eneo la
tukio na sasa wameingia ndani ya majengo ya chuo hicho ambapo kumekuwa
na ufyatulianaji wa risasi kati ya washambuliaji na maafisa wa jeshi.
Waislamu
na wakristo waliotekwa ndani ya Jumba hilo la Chuo kikuu cha garissa
wamedaiwa kutawanywa kabla ya waislamu 15 kuwachiliwa huru kulingana na
msemaji wa kundi hilo la Alshabaab.

kundi la wapiganaji wa Alshabaab limesema kuwa liko ndani ya Chuo hicho kikuu na limewatawanya waislamu na wakristo
Wapiganaji
wamedaiwa kuwateka nyara wanafunzi na kuwaua watu 147 katika chuo hicho
kulingana na wafanyakazi wa msaada na maafisa wa polisi.Takriban watu 65
wengine wamejeruhiwa baada ya washambuliaji kuvamia chuo hicho.

Kundi
la wapiganaji wa Al-shabaab limekiri kutekeleza shambulizi katika chuo
kikuu cha Garissa Kaskazini Mashariki mwa Kenya.

Baadhi ya wanafunzi wamedaiwa kutoroka kutoka mabweni waliokuwa wakilala

Wapiganaji hao wanaodaiwa kuwa watano wanaaminika kuwa ndani ya jengo hilo la Chuo kikuu .

Shirika
la msalaba mwekundu nchini Kenya linasema kuwa watu 30 wamejeruhiwa
huku wanne kati yao wakiwa na majeraha mabaya..Kwa sasa shirika hilo
linawasafirisha madaktari katika eneo hilo.
.BBC Swahili

إرسال تعليق