|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb)
wa katikati alipokuwa anaingia kwenye uwanja uliotumika kumwapisha
Waziri Mkuu mpya wa Lesotho, Mhe. Pakalitha Mosisili jijini Maseru jana.
wengine katika picha, kutoka kulia ni Bibi Talha Mohammed, Afisa kutoka
Wizara ya Mambo ya Nje na Mhe. Radhia Msuya, Balozi wa Tanzania nchini
Afrika Kusini ambaye pia anawakilisha Lesotho. kutoka kushoto ni Maafisa
wa Serikali ya Lesotho. |
|
Waziri
Mkuu mpya wa Lesotho, Mhe. Mosisili (kushoto) akikabidhiwa Bendera ya
nchi hiyo na Waziri Mkuu wa Zamani, Mhe. Thom Thabane kama ishara ya
kukabidhiwa rasmi madaraka ya uwaziri Mkuu. |
|
Waziri Mkuu mpya wa Lesotho, Mhe. Pakalitha Mosisili akitoa neno la shukrani baada ya kuapishwa. |
|
Viogozi
mbalimbali wa Lesotho na kutoka nje ya Lesotho, mwenye kofia nyeupe ni
mke wa mfalme wa Lesotho akiwa na mumewe ambaye ni Mfalme wa Lesotho. |
|
Mandhari ya Uwanja livyokuwa wakati wa sherehe za uapisho. |
|
Waziri
Membe (katikati) alipokuwa anawasili katika Uwanja wa Ndege wa Maseru
kwa ajli ya kushiriki sherehe za uapisho. Mwingine ni Balozi wa Tanzania
mchini Afrika Kusini, Mhe. Bibi Radhia Msuya. |
|
Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Jacob Zuma akiwasili Lesotho kwa ajili ya kushiriki sherehe za uapisho. |
|
Rais Mteule wa Namibia, Mhe. Hage Geingob naye akiwasili Lesotho kwa ajili ya sherehe za uapisho. |
|
Waziri Membe akihojiwa na Mwandishi wa Habari wa TBC, Bw. Stanley Ganzel mara baada ya sherehe kukamilika. |
Nchi
za Afrika zimetakiwa kujifunza kutoka Lesotho, nchi ambayo dunia
inashuhudia imekuwa na utaratibu wa kubadilishana madaraka kwa utulivu
na amani bila fujo za aina yoyote. Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb)
wakati wa sherehe za kumuapisha Waziri Mkuu mpya, Mhe. Pakalitha
Mosisili zilizofanyika jijini Maseru siku ya Jumanne tarehe 17 Machi
2014. Waziri Membe alimwakilisha Rais Jakaya Kiwete katika sherehe hizo.
Mhe.
Mosisili amerudi madarakani baada ya Chama chake cha Democratic
Congress (DC) kuungana na vyama vingine sita vidogo kuunda Serikali ya
Mseto. Mhe. Mosisili alikuwa Waziri Mkuu wa Lesotho kwa miaka 15 (1998 –
2012) na amerudi madarakani katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28
Februari 2015. Uchaguzi huo ulifanyika mapema kwa miaka miwili kutokana
na matatizo ya kisiasa yaliyosababisha kuvunjika kwa Serikali ya Mseto
iliyokuwa inaongozwa na Waziri Mkuu wa Zamani, Mhe. Thom Thabane.
Katika
hotuba yake, Mhe. Mosisili alisema kuwa nchi hiyo inakabiliwa na
changamoto nyingi, hivyo, aliahidi kutumia uzoefu wake kuhakikisha kuwa
nchi inaondokana na migogoro ya kisiasa ili iweze kusonga mbele
kiuchumi.
Viongozi wengine waliohudhuria sherehe hizo ni pamoja na Rais wa Afrika Kusini, Mhe.
Jacob Zuma, Rais Mteule wa Namibia, Mhe. Hage Geingob na Katibu
Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrka (SADC),
Dkt. Stergomena Tax.
No comments:
Post a Comment