Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Wananchi limewakamata
Wahamiaji haramu 64 raia wa nchi ya ETHIOPIA (Wahabeshi) katika Kijiji
cha KIDOKA, Kata ya KIDOKA, Tarafa ya GOIMA, Wilaya ya na CHEMBA na Mkoa
wa DODOMA, mmoja kati yao alikutwa akiwa amefariki dunia aliyetambuliwa
kwa jina moja la TAJIRU anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 –
30. Watu hao walikuwa wakisafirishwa kwa Lori lenye namba za usajili
T.353 AYW Mitsubishi Fuso lililokuwa likiendeshwa na OTHMAN YUNUS
MTEKATEKA, miaka 45, na Mkazi wa ILALA Jangwani jijini Dar es Salaam
akitokea Moshi - Kilimanjaro kwenda mkoani Mbeya.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID
MISIME – SACP amesema Mnamo tarehe 14/03/2015 saa 01:00 asubuhi katika
kijiji cha KIDOKA walionekana watu wengi wasiofahamika wakiwa
wamejificha katika vichaka na mashamba ya watu.
Watu
hao walionekana dhaifu, walikuwa wakila mahindi mabichi na wengine
wakiomba kwa wanakijiji waliokuwa wakipita maeneo jirani msaada wa
chakula na maji ya kunywa kwa ishara, kwa kuwa hawakuwa na uwezo wa
kuongea lugha ya Kiingereza wala Kiswahili.
Kamanda
MISIME amefafanua zaidi kwa kusema wanakijiji walitoa taarifa kwa
uongozi wa kijiji na Jeshi la Polisi, ndipo msako wa kuwakamata
ulifanyika na kufanikia kuwakamata watu hao waliotambuliwa kuwa ni raia
wa nchi ya ETHIOPIA ambao hawakuwa na vibali vya kuingia/kusafiria.
Aidha katika msako huo alikamatwa dereva wa gari hilo aitwaye OTHMAN
YUNUS MTEKATEKA, 45yrs na mkazi wa Ilala Jangwani jijini Dar es Salaam
na baada ya kuhojiwa alikiri kuwa yeye ndiye aliyekuwa anawasafirisha
watu hao akiwa na wenzake wanne ambao walitoweka baada ya gari
kuharibika.
Na
kwamba aliwapakia watu hao tangu tarehe 12/03/2015 huko Moshi –
Kilimanjaro kuwapeleka Mkoani Mbeya kwa kupita njia za panya. Baada ya
gari kuharibika tarehe 14/03/2015 saa 07:00 usiku katika Kijiji cha
Kidoka waliwashusha na kuwapeleka porini kuwaficha kisha kuendelea
kutengeneza gari na iliposhindikana waliwatelekeza porini na gari
kulitelekeza kijijini.
Kamanda MISIME amewataja wahamiaji haramu hao 63 waliokamatwa kuwa ni:-
Uchunguzi zaidi unaendelea ili kuwabaini wahusika wa mtandao huu wa usafirishaji haramu wa binadamu.
Aidha
Kamanda MISIME anawashukuru wananchi wakazi wa kijiji cha Kidoka kwa
ushirikiano waliouonyesha. Aidha ametoa wito kwa Wananchi kutoa taarifa
kwa Jeshi la Polisi na kufichua wahalifu wanaofanya biashara haramu ya
usafirishaji haramu wa Binadamu na madereva wasiwe na tamaa mbaya
kufanya usafirishaji haramu wa binadamu.
Sehemu ya Wahamiaji haramu 64 raia wa nchi ya ETHIOPIA (Wahabeshi)
No comments:
Post a Comment