Mamlaka
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) imekutana na wadau wa viwanda vya
umeme na magari jijini Dar es Salaam kujadili utekelezaji wa mradi wa
mafunzo yanayotolewa na VETA kwa kushirikiana na viwanda ujulikanao kama
Dual Apprenticeship Training Project.
Mradi
huo uliopo kwenye majaribio tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011 kwa
ushirikiano kati ya Hamburg Chamber of Skills Craft ya Ujerumani na
VETA,unalenga kuandaa idadi kubwa ya mafundi stadi wenye ujuzi zaidi kwa
vitendo kwa kuwa sehemu kubwa ya mafunzo hayo inafanyika viwandani.
Akifungua
rasmi warsha hiyo mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi-VETA Leah
Lukindo alisema kwamba ni muhimu kwa vyuo vya ufundi stadi kutoa stadi
zinazohitajika na viwanda kwa kuwa viwanda vinategemea nguvu kazi hiyo
ili kufanikisha malengo yake.
Alisema
kukosekana kwa ushirikiano kati ya vyuo vya ufundi stadi na viwanda
kunasababisha malalamiko mara kwa mara kutoka viwandani ya kutoridhishwa
na utendaji kazi wa wahitimu wa mafunzo ya ufundi stadi nchini.
Alisisitiza
kuwa mfumo wa Dual Apprenticeship Training unamwezesha kijana kupata
ujuzi wa fani husika wakati anafanya kazi kwenye kiwanda hivyo
kumuwezesha kwa kiasi kikubwa kujifunza zaidi kwa vitendo na kuendana
na mahitaji ya soko la ajira pmaoja na kupata uzoefu na uelewa wa
mazingira halisi ya kufanyia kazi.
Aliwataka
wenye viwanda kuonyesha ushirikiano kwa kujiunga na mradi huu ambao una
faida kubwa kwao kwani unawasaidia kupata mfanyakazi mwenye ujuzi
unaotakiwa pamoja na uzoefu wa kazi kwa kuwa muda mmwingi wa masomo
anakuwa kwenye kiwanda husika.
Mkurugenzi
wa Mafunzo ya Ufundi Stadi-VETA Leah Lukindo akizungumza wakati
akifungua rasmi warsha hiyo katika ukumbi wa hoteli ya Giraffe-Dar es
Salaam.
Washiriki wa warsha hiyo ambao ni wadau wa viwanda vya umeme na magari wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi.
Mratibu
wa mradi huo Francis Komba akisisitiza jambo kwa washiriki wakati
akiwasilisha mada inayohusu wajibu wa wadau wa viwanda katika
utekelezaji wa mradi.
Meneja
mradi Martin Mac Mahon akiwasilisha mada juu ya utekelezaji wa mradi
tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011 na mikakati iliyopo kuhakikisha mradi
huo unafikia malengo waliyojiwekea.
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia mada mbalimbali zilizotolewa kuhusu mradi.
Mshauri
wa mradi Ahmed Athuman (kulia) akijadili jambo juu ya mradi na Mkuu wa
chuo cha VETA-Dar es Salaam Samuel Ng`andu wakati wa mapumziko.
Washiriki wa warsha wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi Stadi-VETA Leah Lukindo.
No comments:
Post a Comment