Jana
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia kyando Mchechu ameanza ziara yake ya
kutembelea Mikoa ili kuhimiza utendaji kazi wa viwango na kujionea
utekelezaji wa miradi ya nyumba za gharama nafuu katika mikoa
atakayotembelea ya Singida, Shinyanga, Tabora, Kigoma, Sumbawanga,Katavi
na Mbeya. Picha na Muungano Saguya-Shinyanga
Ujumbe
wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukitembelea jengo
la NHC lililoungua mwaka jana mjini Singida ambapo Shirika linajenga
upya jengo jingine katika kiwanja hicho kilichoko katikati ya mji huo.
Ujumbe
wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la
Unyankumi na kupewa maelezo ya mradi wa nyumba za gharama nafuu na
Meneja wa NHC Mkoa wa Singida Bw. Ladislaus Bamanyisa ulipotembelea
mradi huo kukagua ujenzi wake.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akikagua nyumba za gharama nafuu eneo
la Unyankindi Singida na kukuta mmoja wa wanunuzi wa nyumba hizoakiwa
amejenga ukuta usilingana na viwango vilivyowekwa na NHC katika miliki
zake inazojenga.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu na ujumbe wake wakiwa na mfanyakazi
aliyestaafu utumishi wake NHC Dr. Allan Kabogo (wa pili kutoka kulia)
walipomkuta eneo la Misigiri Wilaya ya Iramba akiwa anajishughulisha na
biashara na huduma za kitabibu. Ujumbe huo ulifurahishwa kuona mstaafu
wa NHC anaishi maisha ya furaha na matumaini makubwa.
Meneja
wa NHC Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo akitoa maelezo ya awali kwa
ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu ulipotembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu
zinazojengwa na NHC Wilayani Igunga jana.
Nyumba
za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Igunga zikiwa katika
hatua ya linta tayari kukamilishwa na kuuzwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo
na maeneo mengine watakaohitaji.
Utekelezaji
wa miradi ya ujenzi wa nyumba za gharama za nafuu unaotekelezwa na NHC
katika mikoa 23 hivi sasa unatoa ajira kwa wananchi wanaozunguka maeneo
ya miradi hiyo kama wananchi hawa walivyonaswa na kamera ya NHC Wilayani
Igunga jana.
Meneja
wa NHC Mkoani Tabora Bw. Erasto Chilambo akiwatembeza viongozi wa
Shirika waliotembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu unaotekelezwa na
NHC Wilayani Igunga kwa ajili ya kuuzia wananchi.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akitoa mchango wa kununua sementi kwa
vikundi vya vijana vya Vijana Tujiajiri na Miti ni Uhai Wilayani Nzega
ambavyo vilipewa msaada na NHC wa mashine za kufyatua matofali
yanayofungamana.Vikundi hivyo sasa vinapata kazi za kuwatengenezea
wateja mbalimbali matofali hayo na hivyo kuwa na ajira endelevu.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakionyesha na
Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo ramani yaeneo lililopewa
NHC ili kujenga nyumba za gharama nafuu Wilayani Nzega.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akipewa maelezo na Msimamizi wa
mradi wa nyumba za gharama nafuu Bw. Mwikuka juu ya hatua zilizofikiwa
katika ujenzi wa nyumba 50 zinazojengwa na NHC eneo la Zongomela
Wilayani Kahama.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akisalimiana na mafundi ujenzi
alipotembelea mradi wa nyumba 50 za gharama nafuu zinazojengwa na NHC
eneo la Zongomela Wilayani Kahama.
Mkurugenzi
wa Usimamaizi wa Mikoa na Utawala Bw. Raymond Mndolwa akishiriki ujenzi
wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Kahama mara
baada ya Uongozi wa Shirika kutembelea mradi huo jana.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akisisitiza umuhimu wa kupunguza
gharama za ujenzi wa nyumba za gharama nafuu unaofanywa na NHC ili
kuwawezesha wananchi wengi kumudu bei ya nyumba hizo alipotembelea
nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Kahama ili kuukagua
mradi huo jana.
Mkurugenzi
wa redio Kahama FM Bw. Marco Mipawa akimpa maelezo Mkurugenzi Mkuu wa
NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu alipotembelea studio hizo ili kufafanua
namna wananchi wanavyoweza kununua nyumba za gharama nafuu zinazojengwa
na NHC eneo la Zongomela Wilayani Kahama jana. Ujenzi wa nyumba hizo
utakamilika mwezi Agosti mwaka huu na kuuzwa kwa wananchi.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akiongea na wafanyakazi wa NHC Mkoa wa
Shinyanga(hawapo pichani) akisisitiza watende kazi zao kwa mtizamo wa
kibiashara na kuongeza tija na kwamba hatasita kumuondoa kazini mtumishi
yeyote wa Shirika ambaye atashindwa kufikia malengo aliyopewa.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akibatilisha eneo la kujenga
nyumba ya biashara mjini Singida kwa Msimamizi wa mradi huo kutoka
kampuni ya B.H Ladwa inayojenga jengo hilo. Kwa sasa jengo hilo
litajengwa mbele ya jengo la Singida Motel ili kuweza kuvutia
wafanyabiashara watakaopanga katika jengo
No comments:
Post a Comment