Takribani
watu 18 wamenusurika kufa leo baada ya gari la abiria lenye T 349 C XB la kampuni ya Sharoni liliokuwa linatoka Arusha kulekea Singida na Dodoma kuanguka
katia eneo la Kisongo jirani na uwanja wa Ndege Jijini Arusha.
Kwa
mujibu wa abiria walikuwa ndani ya basi hilo wamesema kuwa ajali hiyo
imetokea baada ya dereva wa basi hilo kutaka kupita gari lililokuwa
mbele yake bila kuchukua tahadhari na ndipo gari hilo lilipo acha njia
kupinduka.
Kwa
upande wa abiria wa basi hilo aliteyejitambulisha kwa moja la Mama
Latifa amesema gari hilo lilipoteza muelekeo kuwa mara baada ya gari
hilo kufeli breki za nyuma.
Aidha
majeruhi watukio hilo wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospital ya
Rufaa Maunt Meru Jijini Arusha na wengine wameendelea na safari huku
jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa ajali hiyo iliotokea majira
ya saa moja na nusu leo.
No comments:
Post a Comment