Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wa tatu
kulia na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya wa kwanza kushoto
wakikagua mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za makazi zinazojengwa na
Shirikia la Nyumba la Taifa (NHC) katikati ya Manispaa ya Sumbawanga
tarehe 26/03/2015. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Ndugu
Nehemia Mchechu nyumba hizo ambazo ni za ghorofa moja zitauzwa baada ya
kukamilika ujenzi wake kwa njia ya fedha taslimu na njia ya Mikopo ya
benki.
Waziri
wa Ardhi Mhe. William Lukuvi katikati akiweka jiwe la msingi mradi wa
ujenzi wa nyumba 20 za makazi zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa
Mjini Sumbawanga kwa kushirikiana na viongozi wengine wa chama na
Serikali Mkoani Rukwa tarehe 26/03/2015.
Waziri
wa Ardhi Mhe. William Lukuvi kushoto akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Nyumba la Taifa Ndugu Nehemia Mchechu katika hafla fupi ya
uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa nyumba za makazi za shirika
hilo Mjini Sumbawanga.
Michoro ya mradi huo.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na
wananchi (hawapo pichani) wenye malalamiko mbalimbali yanayohusu
migogoro ya ardhi Mkoani Rukwa katika ukumbi wa RDC Mjini Sumbawanga tarehe 26/03/2015.
Mhe. Lukuvi aliwatangazia wananchi wenye malalamiko sugu wamuandikie
wakiambatisha na vielelezo husika na kuviwasilisha kwake ili aweze
kuvifanyia kazi, alisema kuwa "..ni muda sasa wa kuponya mioyo ya watu
ambao wamezulumika kwa muda mrefu..." Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Eng. Stella Manyanya.
Mzee
Julius Nkana Mkazi wa Sumbawanga akiwasilisha malalamiko yake ya mdomo
na maandishi kuhusu mgogoro wa ardhi kwa Mhe. William Lukuvi. Kwa mujibu
wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya Migogoro takribani yote
iliyowasilishwa ilionekana kuibuka kutokana na maeneo mengi yasiyo rasmi
ambayo hayajapimwa na kupewa umiliki unaotambulika kisheria. Aliongeza
kuwa ipo haja kubwa ya Serikali na mamlaka husika kuimarisha eneo la
upimaji wa maeneo na kutoa umiliki wa ardhi kuazia viwanja vya makazi na
mashamba kuepusha migogoro ya kuzulumiana ardhi ambayo imekua ikiua
kwa kasi siku hadi siku.
Waziri
wa Ardhi Mhe. William Lukuvi kulia akipokea malalamiko ya maandishi ya
migogoro ya ardhi kutoka kwa wananchi wa Mkoa wa Rukwa waliopanga mstari
katika ukumbi wa RDC.
Zoezi
hilo liliambatana na mahojiano mbalimbali ambapo kwa wale wenye
malalamiko ambayo kesi zake zipo mahakamani na hazijatolewa uamuzi
walishauriwa kuendelea na kesi zao mpaka zitakapomalizika, Ama kwa wale
ambao kesi zao zinatatulika zitafanyiwa kazi na Wizara ya ardhi ambapo
Waziri husika Mhe. William Lukuvi aliahidi kujibu barua zao za
malalamiko, Malalamiko hayo pia yatafanyiwa kazi na Ofisi ya Kamishna wa
Ardhi nyanda za juu kusini, Ofisi ya baraza la ardhi Mkoa na Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimuhoji diwani wa Kata ya Kizwite Ndugu Mavazi (kushoto) kuhusu malalamiko ya muwekezaji Ndugu Azizi
Tawaqal (wa pili kushoto) kuhusu madai kuwa wananchi wanamtumia katika
kuuza mashamba yaliyonunuliwa na ndungu Aziz Tawaqal licha ya kuwa
walishalipwa fidia. Kesi hiyo bado ipo mahakamani na Mhe. Waziri
amemuagiza Kamanda wa Polisi Wilaya ya Sumbawanga (OCD) kusimamia sheria
kuhakikisha maeneo hayo hayauzwi na hakuna shughuli yeyote inayoendelea
mpaka kesi iliyopo mahakamani ikamilike na kutoa uamuzi.
No comments:
Post a Comment