Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bado wanaendelea kufika nyumbani kwa marehemu Kapteni John Komba kwa ajili ya kutoa salaam za rambi rambi.
Ratiba ya awali iliyotolewa na familia wamesema mwili wa Marehemu Kapteni Komba utafika saa 10 kwa ajili ya sala kisha mwili utalala hapa nyumbani kwake kwa siku ya mwisho kisha kesho March 02 utaelekea Karimjee kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kisha utasafirishwa kuelekea Songea kwa mazishi.
No comments:
Post a Comment