Pages

March 2, 2015

KILI MARATHON;FABIOLA WILLIAM ANG'ARA KM 45 MJINI MOSHI ,IDADA YAONGEZEKA

Wanariadha wakianza kutimua mbio za Kili Marathon kilometa 42 zilizoanzia na kumalizika kwenye uwanja wa Chuo cha ushirika Moshi

Wanariadha wakianza kutimua mbio za Tigo Kili Half Marathon kilometa 21 zilizoanzia na kumalizika kwenye uwanja wa Chuo cha ushirika Moshi

Meneja wa Kampuni ya Simu za mikononi ya Tigo,Cecile (wa pili kulia)Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini,David Charles wakipata picha na wadau walioshiriki mbio hizo. 

Wanariadha kutoka mataifa mbalimbali wakiwa tayari kukimbiza upepo

Ni mbio tu mchuano mkali kuelekea barabara ya Ushirika wa Neema

Mtanzania Fabiola William aliyeibuka mshindi wa kwanza Kili Marathon wanawake  akimaliza mbio zake na kujinyakulia kitita cha Sh milioni 4


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa wa mbio za Tigo Kili Half Marathon wanawake Grace Kimanzi zawadi ya shilingi milioni mbili kutoka kwa Tigo wadhamini wa mbio hizo.
Habari picha na Rweyemamu info blog 

 
 **************
Mwana dada wa Tanzania Fabiola William (32),ameibuka mshindi wa kilomita 42 (Full Marathon woman) katika mbio za Kilimanjaro Marathon zilizofanyika leo katika viunga vya mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro. 
 
Fabiola ametumia muda wa saa 2:49:51 na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 4 kutoka kwa wadhamini Kilimanjaro Lager na kuwaburuza wakenya Rosaline David, Joan Cherop, Dorice Todipus, Sarah Maiyo , Gladys Cheruiyo , Susan Koskei, Julitter Tanin, Esther Mutuku na Lilian Chelimo walioshika namba 2 hadi 10.
 
Full Marathon wanaume, David Ruto (Kenya), aliibukamshindi baada ya kutumia 2:15:50 na kuzawadiwa Sh milioni 4 huku nafasi ya pili hadi ya tano zikienda Kenya kwa wakimbiaji, Benard Kimayo, Alex Bartida,  George Ngure na Douglas Chebii.
 
Mtanzania Pascal Mombo alijitokeza na kushika nafasi ya sita huku wakenya David Kilimo, Lawrence Rotich, Mathew Koskei wakichukuanafasi ya 7 hadi 9 na Mtanzania Siegried Ngolly kumaliza wa kumi.
 
Aidha katika mbio za Kilomita 21, nafasi ya kwanza hadi ya nne ilikwenda kwa Watanzania,  Ismail Juma, Emmanuel Giniki, Theotil Joseph, Felix Alfonse huku nafasi tano hadi ya nane ikienda Kenya kupitia  Festus Stalamestus, Vicent Kipruto, Fanuel Mkungo na Dickson Kimuthi, Mtanzania Elia Sidame alimaliza wa tisa na mkenya Martin Muhinde kumaliza wa kumi.
 
Upande wa wanawake Half Marathon Kilomita 21, wakim,biaji wa Kenya walifanya vyema kwa kuchukua tano bora ikiongozwa na Grace Kimanzi ,Yunice Echumba, Vicoty Cherkemai, Sherekith Nyawera, Jane Mwikal.
 
Nafasi ya sita hadi ya nane ilikwenda kwa watanzania  Failuna Abdi, Mary Naali na Catherine Lange na tisa na kumi zikenda Kenya Yunice Mutie na  Ludera Fida.
 
Akizungumza katika mbio hizo, mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe, alisema aliwapongeza waandaaji wa tukio hilo la aina yake.

“Nawapongeza sana wadhamini wakuu Kilimanjaro Premium Lager, waandaaji na wadau mbalimbali ambao kwa pamoja mmefanikisha mbio hizi kwa miaka 13 sasa,” alisema.

Pia aliwapongeza GAPCO kwa kudhamini mbio za walemavu pamoja na wadhamini wengine ikiwemo Grand Malt, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar,  CMC Automobiles Ltd, RwandAir, FNB Tanzania, Kibo Palace Hotel, UNFPA, Kilimanjaro Water, pamoja na wadhamini shirikishi wapya kabisa katika  mbio hizi ambao ni NSSF na Tanzania Coffee Board.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...