Ama
kweli ukistaajabu ya musa hakika utayaona ya firauni...na kuishi kwingi
ni kuona mengi...hali kadhalika wahenga wanasema Tembea uyaone...Misemo
hiyo mitatu inaweza kujidhihirisha kwa namna tofauti tofauti kupitia
tukio la mkazi wa Jiji la Dar es salaam ambaye ni Mwalimu wa kike katika
shule ya Sekondari Kibasila iliyopo hatua kadhaa kutoka Manispaa ya
Temeke kubainika ndani kwake alipokua akiishi huko Yombo,
Kisiwani Kata ya Sandari kuwa kuna shehena ya kinyesi cha binadamu
katika ndoo, mabeseni, chupa za soda, maji pamoja na majagi.
Pichani
juu ni Wafanyakazi wa usafi wa Manispaa ya Temeke wakibeba kinyesi
kwenda kukimwaga baada ya kuvunja nyumba aliyokuwa akiishi Mwalimu
Gaudencia Albert.
Ubebabi kinyesi ukiendelea
Shehena ya kinyesi iliyokuwa chumbani kwa mwalimu huyo.
********
Manispaa ya Temeke jana Februari 25, 2015, imeteketeza kinyesi kilichokutwa
katika chumba cha mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila Gaudensia Albert
baada ya maofisa wa afya wa manispaa hiyo kuchukua hatua hiyo ili kunusuru afya
za wakazi wa eneo hilo.
Kazi hiyo ilifanyika majira ya saa tisa alasiri katika eneo
la Yombo, Kisiwani Kata ya Sandari jijini Dar es chini ya uangalizi wa Jeshi la
Polisi na wakishirikiana na Mwanyekiti wa Mtaa huo, Yahya Bwanga.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini wakati wa zoezi
hilo, Ofisa Afya wa Manispaa ya Temeke, Floyd Tembo alisema tukio hilo
walilipata juzi juzi jioni, baada ya kulipata waliwatuma Watendaji wa Afya wa
Kata hiyo wafanye utafiti wakujua tatizo hilo lilikuwa na ukubwa gani. SOMA ZAIDI KWA KUBOFYA HABARI MSETO BLOG
No comments:
Post a Comment