Wakati
serikali ikihaha kutafuta muarobaini wa mauaji ya watu wenye ulemavu
Ngozo (Albino), katika mikoa ya kanda ya ziwa huku ikidiriki kutangaza
vita dhidi ya wapiga ramli wote, katika hali isiyokuwa ya kawaida
imebainika kuwa watoto ambao huzaliwa wakiwa hawajafikisha umri na kufa
au kupoteza maisha wakati wa kuzaliwa viungo vyao huuzwa kwa waganga wa
kienyeji katika hospitali ya wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.
Inaelezwa kuwa
akina mama wanaojifungua watoto hao na kwa bahati mbaya kupoteza maisha,
viungo vya watoto hao huwa havipelekwi kuzikwa kama ilivyo kawaida na
taratibu za hospitali, badala yake wauguzi na wafanyakazi wengine
huchukua viungo hivyo na kupeleka kwa waganga wa jadi.
Tuhuma hizo zilitolewa juzi mbele ya
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Mwamvua Jilumbi katika kikao cha pamoja
na wadau wa afya mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa kanisa la KKKT
mjini Bariadi wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa kukomesha vifo vya
wajawazito na watoto mkoani Simiyu ulioko chini ya AMREF Tanzania.
Wadau hao walibainisha kuwa hali
hiyo imekuwa ikijitokeza kila mara katika hospitali ya Wilaya ya Bariadi
Mkoani Simiyu, ambapo walieleza kuwa mtandao mzima wa kuuzwa kwa viungo
hivyo ufanyika kati ya wauguzi pamoja na madaktari ambao ndiyo wahusika
wakuu kuzalisha akina mama wajawazito.
Mbele ya Katibu huyo tawala wa Mkoa
wadau hao waliendelea kueleza kuwa viungo hivyo vimekuwa vikiuzwa
kuanzia shilingi 400,000 hadi 500,000 kiasi ambacho walieleza hutolewa
na waganga wa hao wa jadi.
“..katika hospitali yetu ya Bariadi
kuna jambo ambalo siyo zuri na jema leo ngoja tulitoboe mbele ya kikao
hiki na tena mbele za waandishi wa habari na wewe Katibu tawala wa
Mkoa..akina mama wanaojifungua watoto wao kwa bahati mbaya akafariki
viungo vya watoto hao huuzwa kwa waganga wa jadi” Alisema Gasper Mathew
na kuongeza kuwa.
.
“ viungo hivyo vinauzwa shilingi
400,000 hadi 500,000 huu ni ushirikina wa hali ya juu na ni
hatari..wauguzi pamoja na madaktari ndiyo wanahusika sana..wamekuwa
wakipewa kiasi hicho..kila mara wanafaya hivyo lakini tumekuwa kimya”
Alisema
Walisema kuwa akinamama wengi
hufika hospitalini hapo kwa lengo la kujifungua na mara wanapojifungua
na kwa bahati mbaya mtoto au watoto kufariki kutokana na matatizo ya
afya ya uzazi baadhi huamua kuwahifadhi katika chumba cha maiti lakini
wengi hujikuta wakirejea nyumbani mikono mitupu baada ya miili ya watoto
wao kuuzwa kwa waganga wa kienyeji.
Akizungumzia tuhuma hizo Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Mwamvua Jilumbi katika kikao hicho alimtaka
Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mji wa Bariadi Erica Masika kutoa maelezo
juu ya tuhuma hizo.
Akitoa maelezo ya tuhuma hiyo
Mkurugenzi huyo alisema kuwa hana taarifa yoyote juu ya kuwepo kwa
vitendo hivyo katika hospitali yake, huku akieleza kuwa watafanya
uchunguzi mara moja na watakao bainika kufanya hivyo watachukuliwa
sheria mara moja.
“..hii ni hatari mimi hili
nimelipata hapa na nimelisikia leo sina taarifa yeyote.. ila nawaomba
wadau waliotoa tuhuma hizi tushirikiane tufanye uchunguzi haraka ili
tuwabaini na watakaobainika tutawachulia sheria za kinidhamu” Alisema
Mssika.
Katika kikao hicho Meneja Mradi wa
Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na masula ya afya AMREF
Health Africa tawi la Tanzania,katika mkoa wa Simiyu, Godfrey Matumu,
aliitaka jamii ya mkoa wa Simiyu kushiriki kikamilifu katika kuthibiti
vifo vya akinamama wajawazito na watoto wachanga wenye umri chini ya
miaka mitano.
Alisema vifo hivyo vimekuwa
vikisababishwa na kuchelewa kupata huduma katika vituo vya afya kwa
wakati.wakati wa kuzindua Mpango Mkakati wa Huduma za Afya ya Uzazi na
Mtoto katika mkoa wa Simiyu utakaotekelezwa kwa muda wa miaka 4
(2014-18),chini ya msaada wa watu wa Canada. Chanzo-http://simiyunews.blogspot.com
No comments:
Post a Comment