Mshindi
wa Milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na
Vodacom Tanzania,Uwezo Magedenge (22) akiwa nyumbani kwao kijiji cha
Pamilini Kilolo Mkoa wa Iringa akiendelea na shughuri zake za nyumbani
wakati alipotembelewa na maofisa wa Vodacom Tanzania kijijini hapo kwa
ajili ya kumchukua na kumpeleka jijini Dar es Salaam kwa makabidhiano
rasmi ya kitita chake hivi karibuni.
Meneja
Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (kulia) akimsikiliza
kwa makini mshindi wa milioni 100/-kupitia promosheni ya JayMillions
inayoendeshwa na kampuni hiyo Bi.Uwezo Magedenge (22) akimfafanulia
jambo kuhusiana na ushindi wake,wakati alipomtembelea kijijini kwao
Pamilini Kilolo mkoa wa Iringa kwa ajili ya kumchukua na kumpeleka
jijini Dar es Salaam, kwa makabidhiano rasmi ya kitita chake hivi
karibuni.Wengine katika picha kushoto ni Mama yake mzazi Delfine
Kisoma(64) na Baba yake Alatanga Magendenge (70).
Baba
mzazi wa mshindi wa kwanza wa milioni 100 kupitia promosheni ya
JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Alatanga Magendenge
akimfafanulia jambo Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu(kulia)
kuhusiana na ushindi wa mwanae Uwezo Magendenge(watatu toka
kushoto)wakati alipomtembelea mshindi huyo nyumbani kwao kijiji cha
Pamilini Kilolo Iringa kwa ajili ya kumchukua na kumpeleka Dar es
Salaam kwa ajili ya kumkabidhi rasmi ya kitita chake hivi
karibuni,kushoto ni mama mzazi wa mshindi Delfine Kisoma.
Mshindi
wa Milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na
Vodacom Tanzania,Bi. Uwezo Magedenga (kushoto) akifurahia jambo na
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)wakati
alipofika kijijini kwao Pamilini Kilolo Iringa ili kujua mazingiara
yake na kumpeleka jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya
kumkabidhi rasmi ya kitita chake hivi karibuni. Katikati ni Mkuu wa
kampuni hiyo Kanda ya Kusini magharibi Amos Vuhahula.
Mshindi
wa kitita cha shilingi Milioni 100/-kuptia promosheni ya JayMillions
inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Uwezo Alatanga Magedenge (22)
akifafanua jambo kuhusiana na ushindi wake wakati alipotembelewa na
maofisa wa Vodacom Tanzania kijijini kwao Pamilini Kilolo Iringa.
Mshindi
wa kwanza wa kitita cha shilingi milioni 100/-kupitia promosheni ya
Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Uwezo Magedenga katikati
akiwa kwenye picha ya pamoja na wazazi wake,Alatanga Magedenga na
Delfina Kisoma(kushoto) nje ya nyumba yao iliyopo katika kijiji cha
Pamilini Kilolo mkoa wa Iringa .
Wazazi
wa mshindi wa kwanza wa Sh Milioni 100 katika droo ya 14 ya promosheni
ya Jaymilioni inayoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom, Uwezo
Magendenye (22) mkazi wa wilaya ya Kilolo wamesema kuwa wamefurahishwa
na ushindi wa binti yao na watamshauri kuhakikisha anazitumia kuboresha
maisha yao na kutimiza ndoto zake alizoshindwa kuzitimiza kutokana na
familia aliyozaliwa kutokuwa na uwezo.
Baba
mzazi wa binti huyo, mzee Alatanga Madengenye (70),alionyesha furaha
kubwa alipotembelewa na maafisa wa kampuni ya Vodacom na kusema kuwa
hatapenda kumuingilia kwenye matumizi ya pesa hizo japokuwa kama mzazi
angependa kuona binti yake anatimiza na ndoto yake aliyoikosa kutoka na
hali ngumu ya maisha inayowakabili ambayo ni kuhakikisha anapata
elimu bora.
“Binti
yetu bado ni mdogo tuna imani kwa ushindi huu atarudi shule kwa ajili
ya kujiendeleza kimaisha”.Alisema Mzee Madengenye akiungwa mkono na mama
yake mzazi Delfina Kisoma (64) alielezea furaha yake juu ya ushindi wa
binti yake huyo akisema ni matarajio yao ushindi huo utasaidia kubadili
maisha ya binti huyo na familia yao.
Akizungumza
namna fedha hizo zitakavyobadili maisha yake, Uwezo Madengenye alisema
kwa furaha na kujiamini alisema sasa ameamua kurudi shule kutafuta elimu
aliyoikosa kutokana uwezo mdogo wa kifedha wa wazazi wake.“Ndoto
yangu ya kurudia mitihani ya kidato cha nne iliyokufa miaka miwili
iliyopita kutokana na uwezo mdogo wa familia sasa imefufuka. Nitarudi
shule, nitasoma kwa bidii hadi nipate shahada ya chuo kikuu kama
itawezekana,” alisema.
Alitaja
matumizi mengine atakayofanya kuwa ni pamoja na kununua ardhi na
kupanda miti, kukarabati nyumba ya wazazi wake na kusaidia ndugu zake
ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaisha ikiwemo
kuanzisha biashara za aina mbalimbali ikiwemo biashara ya maduka ya
M-Pesa na ikibidi kujenga nyumba yake ya kulala wageni .
Meneja
Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu alitembelea familia
ya mshindi huyo akiongozana na Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi wa
kampuni hiyo Amos Vuhahula alisema binti huyo atakabidhiwa fedha zake
jijini Dar es Salaam baada ya taratibu za makabidhiano kukamilika na
aliwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni hiyo kwa kuhakikisha
wanatuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za
kushinda.
Aliitaja
njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544
iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi
300/-
Alisema
tangu promosheni hiyo ianze mapema mwezi uliopitau tayari wateja 2
wamekwishajishindia milioni 10 na wateja watano wameishajishindia
shilingi milioni moja kila mmoja na maelfu wengine tayari
wamejishindia muda wa maongezi.
“Promosheni
hii itadumu kwa muda wa siku mia moja, bado kuna mamilioni ya fedha
yanawasubiri watanzania, wanachopaswa kufanya ni kuhakikisha kila siku
wanaangalia kama namba zao zimeibuka na ushindi kwenye droo ya siku kwa
kutuma neno Jay kwenda namba 15544.
No comments:
Post a Comment