Mhe.
Prof. Mark Mwandosya akifafanua jambo wakati wa mkutano wa pamoja na
Waziri wa Maji na Umeme wa Sudan Mhe Mutaz Moussa Abdallah Salim.
Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bwana Felix Ngamlagosi ambaye
ameongozana pamoja na maafisa wengine na Waziri Prof. Mwandosya
Mhe.
Prof. Mark Mwandosya akitoa maelezo katika mkutano wa pamoja na Waziri
wa Maji na Umeme wa Sudan Mhe Mutaz Moussa Abdallah Salim.
Ujumbe
wa Tanzania ukiongozwa na Mhe. Prof. Mark Mwandosya katika mkutano wa
pamoja na ujumbe wa Sudan ulioongozwa na Waziri wa Maji na Umeme wa
Sudan Mhe Mutaz Moussa Abdallah Salim.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Mhe. Prof. Mark Mwandosya
akikaribishwa na mwenyeji wake Waziri wa Maji na Umeme wa Sudan Mhe.
Mutaz Moussa Abdallah Salim mara alipowasili katika Ofisi za Wizara hiyo
Jijini Khartoum.
……………………………………………………………………………………………………………………………………..
12 – 17 JANUARI 2015 Mheshimiwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya yuko
ziarani nchini Sudan ambako atatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo
nchini humo ikiwemo miradi mikubwa ya mabwawa yaliyojengwa katika bonde
la Mto Nile pamoja na kubadilishana uzoefu na taasisi za Sudan
zinazojihusisha na udhibiti wa huduma katika sekta za maji, nishati,
mawasiliano na usafirishaji.
Ujumbe wa Mhe. Prof. Mwandosya umejumuisha wataalamu kutoka Wizara ya Maji, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA).
Mhe. Prof. Mwandosya alianza ziara yake Jumatatu ya tarehe 12 Januari, 2015 kwa kutembelea Wizara ya Rasilimali za Maji na Nishati ya Umeme ya Jamhuri ya Sudan.
Katika
ziara hiyo Mhe. Prof. Mwandosya alieleza kuwa pamoja na shughuli
zingine, ameandamana na taasisi za udhibiti kutoka Tanzania ili
kujifunza na kubalishana uzoefu katika shughuli za udhibiti kutoka kwa
taasisi kama hizo katika nchi ya Sudan.
Waziri
alieleza kuwa shughuli za udhibiti Tanzania zimekuwa zikifanyika kwa
kipindi cha takribani miaka 10 sasa. Waziri alieleza kuwa pamoja na
mafanikio yaliyopatika katika kutekeleza majukumu yao, Mamlaka za
Udhibiti bado zina changamoto nyingi ambazo inabidi kukabiliana nazo kwa
kujifunza na kubadilisha uzoefu na taasisi kama hizo katika nchi kama
Sudan.
No comments:
Post a Comment