Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na viongozi wa mkoa wa Katavi kwenye
uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya ziara yake ya jimbo la uchaguzi
Januari 9, 2015. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Pazi
Mwamlima, Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Emmanuel Kalobelo na
Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Kanali Ngemera Lugunga.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiangalia msokoto wa rasta isiyokuwa ya kawaida
aliosuka Bwana huyo, baada ya kuwasili kwenye uwanja wa shule ya ufundi
ya Mamba wilayani Mlele kuhutubia mkutano wa hadhara Januari 9, 2015.
Sungusungu
wa tarafa ya Mamba wilayani Mlele wakicheza ngoma wakati Mbunge wao,
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipowasili kwenye uwanja wa Shule ya Ufundi
ya Mamba kuhutubia Mkutano wa hadhara Januari 9, 2015.(Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment