Pages

January 17, 2015

VANESA MDEE ACHAGULIWA KUWA BALOZI WA SAMSUNG TANZANIA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Ya Samsung Tanzania Mike Seo akibadilishana Mkataba na Msanii Vanessa Mdee pamoja na Meneja wake Michele Baldini.
 Vanessa Mdee akiwa katika picha ya Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Samsung Tanzania Mike Seo, Silvester Manyara Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania pamoja na Meneja wa Vanessa Mdee Michele Baldini
 Mike Seo Mkurugenzi Mtendaji wa Samsung Tanzania akimkabidhi simu msanii wa Muziki Tanzania Vanessa Mdee
 Mike Seo Mkurugenzi Mtendaji wa Samsung Tanzania akitia Saini Mkataba wa makubaliano baina yao na Msanii Vanessa Mdee
 Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania akiongea na wanahabari 
Vannessa Mdee akiongea na wanahabari 
Dar es Salaam, 16 Januari 2015; Kampuni ya kielektroniki ya Samsung kwa mara ya kwanza imehusisha kampuni hiyo na msanii wa muziki kutoka nchini Tanzania. Leo hii, Kampuni namba moja duniani inayoongoza kwa technolojia ya hali ya juu, Samsung wanayo furaha kumtangaza balozi wao mpya mwanamziki nyota, na mtangazaji wa Televisheni na radio Vanessa Mdee.
Katika mkutano na wanahabari ulilofanyika hoteli, ya Hyatt Regency, iliyoko  mjini Dar es Salaam iliohusisha kusaini kwa mkataba baina ya Vannesa Mdee na uongozi wa kampuni ya Samsung ni ishara  tosha ya makubaliano rasmi kati ya Kampuni ya Samsung na msanii huyo. Kitendo hicho  kilihashiria  mwanzo wa kazi mpya kwa Vanessa Mdee kama mwakilishi wa kampuni ya  Samsung nchini Tanzania.
Akiwa kama balozi wa kampuni ya Samsung, Vanessa atakuwa kiungo muhimu katika muonekano na uzinduzi wa bidhaa mbalimbali za kampuni hiyo.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kielektroniki ya Samsung, Mheshimiwa Mike Seo alisema kuwa, "kwa kutambua  ongezeko la uhitaji wa simu za kisasa kwa soko la kati nchini Tanzania ni bora kuwasiliana na wateja wetu kupitia  mtu ambaye amebeba sifa zinazoendana na vifaa vyetu na soko letu. Anaongeza kuwa "Tunafuraha sana kutangaza ushirikiano wetu na Vanessa Mdee akiwa kama Balozi wetu mpya nchini Tanzania. Akiwa kama mwanamziki nyota na mchangiaji chanya kwa wananchi wa Tanzania. Vanessa anawakilishi vijana wa kisasa wa Tanzania na ni  mtu ambaye kampuni ya Samsung inaweza kufanya naye kazi hivyo basi tunafuraha kubwa kuwa na mtu kama huyu kuwakilisha bidhaa zetu. "
Vanessa Mdee ambaye aliongozana na menejimenti yake kwenye mkutano huo, alielezea juu ya furaha yake kwa kuwa sehemu ya kampuni ya Samsung, alisema "Samsung ni kampuni kubwa na yenye hadhi ya juu, ni heshima kubwa sana kwangu kuwa balozi wa kampuni hii inayoongoza kwa kutengeneza vifaa vya kielektroniki ulimwengu, huu ni mwanzo tu wa jinsi mwaka 2015 utakavokuwa wa mafanikio kati yangu na kampuni ya Samsung. Binafsi, natumaini juu ya kazi hii na nasubiri kwa hamu siku nitakayoanza kazi rasmi. "

Kuhusu ya Samsung .

Samsung Electronics Co., Ltd. Ni kampuni gwiji la vifaa vya kieletroniki linalofungua milango kwa watu duniani.  Kupitia uvumbuzi na ugunduzi tunabadilisha ulimwengu wa TV, simu za kisasa, tablets, kompyuta, kamera, printa na vifaa vya nyumbani. Na tumetoa jira kwa zaidi ya watu 286,000 katika nchi mbali mbali duniani na makadirio ya mapato yapatayo dola bilioni 216.7. Tembele  tovuti yetu kupata maelezo zaid kuhusu kampeni yetu. www.samsung.com.
Kuhusu Vanessa.

Juu ya mwendo wa kazi zake, muimbaji wa Tanzania, mtunzi wa nyimbo, na mwanamuziki nyota Vanessa ametoa nyimbo tano ikiwa ni pamoja na Closer, Hawajui, Come Over, Wave Clap dance na Siri, pia  ameshirikishwa katika nyimbo kama Me and you na Ommy Dimples, Money na AY, Monifere na Gosy B, Bashasha na Bob Junior na Nisamehe na Angle. Vanessa alishinda tuzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na tuzo nne za Kill Music Awards na moja ya Afrika all Music Award. Amekuwa akijihusisha na kampeni mbalimbali kama vile Staying Alive Foundation Project, kampeni ya Zinduka, MTV Africa Music Awards, Sauti Za Busara, UNAIDS Mkutano wa vijana Mali uliofanyika Bamako, Mkutano wa Kimataifa juu ya VVU na magonjwa ya zinaa ulofanyika Addis Ababa, Ethiopia. Mdee amekuwa akiendesha vipindi kama MTV Base meets, shoo inayolenga kuwawezesha vijana Waafrika kutoka duniani kote kwa kuwapa fursa ya kukaa chini na kiongozi mashuhuri, Kili Music Awards, Epiq Bongo Star Search (EBSS), Dume Challenge, 'Switch On' kampeni ya Airtel, Coke Studio Afrika, Kili Music Tour, Serengeti Fiesta Music Tour, Coca Cola Chart Express, The Hit  ya Choice FM, pan-African TV show na MTV Base select 10. Alishawahi kupata tuzo katika Gala mjini New York kutoka kwa UNA-YP, alituzwa na GAVI Alliance kwa msaada wake katika uanzishwaji wa chanjo bure kwa watoto wa Tanzania. Mdee balozi wa GAVI na mpambanaji dhidi ya kansa ya kizazi. Mwaka 2014 alipata mkataba kutoka kampuni ya Crown Paints, kuwa balozi wake nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment