Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akizunguza na waandishi
wa habari kwenye makao makuu ya tume ya uchaguzi jijini Dar es salaam
wakati alipozungumzia maandalizi ya uboreshaji wa daftari la wapiga
kura, kura ya maoni ya Katiba mpya na uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka
huu, kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Bw. Julius Mh.Julius
Mallaba.
Baadhi ya waadishi wa habari wakiwa katika kutano huo.
.................................................................................................................
Ndugu Waandishi wa Habari,
Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Watendaji wa Tume,
Mabibi na Mabwana.
Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Watendaji wa Tume,
Mabibi na Mabwana.
Kwa niaba
ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, napenda kuchukua fursa hii
kuwakaribisheni kwa mara nyingine katika Mkutano huu. Nawashukuru
kwamba, pamoja na majukumu mengi mliyo nayo, mmeweza kuupa umuhimu wa
pekee mkutano wetu huu na kuhudhuria kwa wingi. Kwa niaba ya Tume ya
Taifa ya Uchaguzi, nasema Ahsanteni na Karibuni sana.
Katika
mkutano huu, Tume inalenga kutoa taarifa kuhusu tathmini ya utekelezaji
wa zoezi la majaribio ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
(Pilot Registration) kwa mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR)
zoezi ambalo lilikamilika wiki iliyopita.
Ndugu Wanahabari,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi, imepewa jukumu la kisheria Kuandikisha Wapiga Kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuliboresha Daftari hilo kwa ajili ya Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani. Kwa mujibu wa Sheria ya Kura ya Maoni, Daftari hili la Kudumu pia litatumika katika Kura ya Maoni kuhusu Katiba Inayopendekezwa.

Ndugu
Wanahabari; mtakumbuka kuwa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa katika
mchakato wa Maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
kwa kutumia Teknolojia Mpya ya "Biometric Voter Registration" (BVR) na
mara kwa mara imekuwa ikiomba kukutana nanyi ili kuwapa taarifa kuhusu
hatua mbalimbali ambazo Tume imekuwa ikizipitia.
Kwa kuwa
Uboreshaji huu ulihusisha matumizi ya vifaa vya teknolojia ya kisasa,
vifaa ambavyo vilikuwa havijawahi kutumika katika Uboreshaji nchini,
tuliona si vyema kuagiza vifaa vingi kabla ya kuvifanyia majaribio.
Zoezi la majaribio lilifanyika ili kuwa na uhakika kuwa vifaa hivi vya
Biometric Registration vina uwezo wa kuandikisha Wapiga Kura katika
mazingira ya nchi yetu. Zoezi hili liliangalia uwezo wa watendaji
kutumia BVR katika uandikishaji na pia uwezo wa vyombo vyenyewe katika
Software na Hardware kwenye uandikishaji. Katika zoezi hili tuliangalia
changamoto zilizojitokeza ili kuzipatia ufumbuzi kabla ya kuanza Zoezi
halisi la Uandikishaji wa nchi nzima.
Ndugu Wanahabari,
Kama nilivyosema, Tume inakutana nanyi ili kuwapa taarifa kuhusu Tathmini ya Utekelezaji wa zoezi la Majaribio la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililofanyika kwa siku saba (7) katika Kata za Bunju na Mbweni katika Jimbo la Kawe, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam; Kata za Ifakara, Kakingiuka, Ipangala, Mlabani na Viwanja Sitini katika Jimbo la Kilombero Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro; na Kata za Ikuba, Usevya na Kibaoni katika Jimbo la Katavi, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.

Tume kwa
namna ya pekee, inawashukuru sana Waandishi wa Habari kwa kujitokeza na
kufuatilia zoezi hili la majaribio ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura. Waandishi wa Habari wamesaidia sana katika kuhamasisha
Wananchi wa Majimbo husika kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Vilevile, Waandishi wa Habari
wamesidia katika kutoa taarifa za maendeleo ya zoezi hili kitu ambacho
kimesaidia kufanikisha zoezi hili.
Jumla ya
BVR Kits 250 zilitumika katika Uboreshaji huo kwa mgawanyo ufuatao:-
Halmashauri ya Kilombero BVR Kits 80, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele BVR
Kits 80 na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni BVR Kits 90. Vituo
katika Kata zote vilikuwa vinafunguliwa saa 2.00 asubuhi na kufungwa saa
12.00 jioni.Ndugu Waandishi wa Habari,
Tume inapenda kuwafahamisha kuwa zoezi hilo la Majaribio ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika majimbo matatu yaliyotajwa limefanyika na kukamilika kwa mafanikio makubwa. Changamoto zilizojitokeza hapa na pale zimetusaidia kupata ufumbuzi ambao utatusaidia wakati wa Uandikishaji wenyewe nchi nzima.

Tunasema
mafanikio makubwa kwa sababu matokeo ya jumla yanaonyesha kuwa idadi ya
wapiga kura waliojitokeza kujiandikisha ilikuwa kubwa na kuvuka malengo
ya waliokadiriwa kuandikishwa.
Mkoa wa
Dar es salaam, Kata za Bunju Wapiga Kura 15,123 waliandikishwa kati ya
27,148 na Kata ya Mbweni Wapiga Kura 6,200 waliandikishwa kati ya 8,278.
Takwimu hizi za waliondikishwa inatokana na makisio ya watu tuliyokuwa
tumejiwekea kutokana na matokeo ya sensa mwaka 2012. Mkoa wa Morogoro
Kata za Ifakara, Kakingiuka, Ipangala, Mlabani na Viwanja Sitini Wapiga
Kura walioandikishwa ni 19,188 wakati makisio yalikuwa watu 17,790 na
Mkoa wa Katavi Halmashauri ya Mlele kata za Ikuba, Usevya na Kibaoni
Wapiga Kura 11,210 waliandikishwa wakati makisio yalikuwa watu 11,394.
Matokeo haya yanadhihirisha kuwa vifaa vya uandikishaji vilifanya kazi
vizuri na hivyo vinaweza kutumika katika Uboreshaji wa Daftari la Kudumu
la Wapiga Kura kwa nchi nzima.
Pamoja na
mafanikio hayo, kama ilivyo kawaida katika majaribio yoyote kwani ndiyo
lengo la kufanya majaribio, zilikuwepo changamoto kadhaa wakati wa
utekelezaji wa zoezi hilo. Changamoto hizo zinaweza kuwekwa katika
makundi makubwa matano kama ifuatavyo:-
i. Matatizo yaliyotokana na 'Settings' za BVR Kits;
• Baadhi ya "BVR Kits" zilitumia camera iliyo katika Laptop badala ya camera iliyowekwa kwa ajili ya kupiga picha.
• Uchukuaji wa alama za vidole (Automatic Process settings) ilisababisha Mfumo kusimama (Crash).
• Tatizo la kuchukua picha iwapo viwango vya ICAO vya ubora wa Picha havijafikiwa kama
• Unrecognise face,
• Unrecognise eye,
• Stretch photo,
• Un even light.
• Uwepo wa Majina yenye "apostrophe".
ii. Matatizo yaliyosababishwa na Software;
• Fingeprint Scanner kusababisha Mfumo wa Uandikishaji kusimama (Crash) kutokana na SDK na za vifaa finger print scanner.
• Kuharibika kwa baadhi ya file (File Corruption) kutokana na d11 ya finger print scanner.
iii. Matatizo ya hardware;
• Komputa (Laptop) Kupata Joto kutokana na Bati liliwekwa kuzuia kuibiwa Laptop kwa urahisi ambapo mahitaji kuwezesha mzunguko wa hewa ndani ya "BVR Kit".
• FlashDrive ya pili (Drive G) kutoonekana hivyo kuhitaji kubadilishwa na kuwa SD card.
• Uharaka wa uchukuaji alama za vidole ambapo ilibidi kufanya mabadiliko.
iv. Matatizo ya lojistiki na matatizo ya Watendaji wa zoezi la Uandikishaji.
• "BVR Kit" kuchelewa kufikishwa katika Vituo.
• Vurugu wakati wa uandikishaji ambao unahitaji Ulinzi kuwepo.
• Baadhi ya "BVR Operator" kutokuwa na uwezo au kuwa makini katika utumiaji wa "BVR Kits" hivyo kuhitaji elimu zaidi kwa "BVR Kit Operator".
• "BVR Kit Operator" kubadili Kits kwa tatizo dogo linaloweza kutatulika kwa urahisi.
• "BVR Kit Operators" kutokuwa na uelewa wa matumizi ya "Solar Panel" kwani baadhi ziliwekwa chini ya mti au kutogeuzwa kadri muda ulivyokuwa unakwenda.

Mbali ya changamoto hizo zilikuwepo pia changamoto nyingine za kimiundombinu na kibinadamu. Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na Hali ya Hewa hususan katika jiji la Dar es salaam na Morogoro. Mtakubaliana nami kuwa pamoja na kuwa jiji la Dar es salaam kwa kawaida lina hali ya hewa ya joto lakini kwa takribani mwezi mmoja hivi uliopita kumekuwa na ongezeko la joto hali iliyosababisha hata baadhi ya vifaa vya kuandikishia hususan 'BVR Kits' wakati mwingine kushindwa kufanya kazi inavyotakiwa na hivyo kusababisha shughuli za uchapishaji wa Kadi za Kupigia Kura kuchelewa.
Aidha, ushirikiano mdogo kutoka kwa Wananchi nao ulikuwa changamoto iliyosababisha zoezi hilo kwenda taratibu. Baadhi ya wananchi kushindwa kuzingatia maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na BVR Kit Operators kutokana na uelewa duni kwani ilibainika pia kuwa bado kuna idadi kubwa ya wasiojua Kusoma na Kuandika. Hali hiyo ilifanya zoezi la Uchukuaji wa alama za Vidole (Fingerprint) na Utiaji wa Saini kuwa mgumu.
Kadhalika
kumekuwepo na mwamko mkubwa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili
kujiandikisha. Hivyo, kulikuwepo na watu wengi sana katika vituo vya
Uboreshaji wa Daftari hilo la Kudumu la Wapiga Kura. Changamoto zote
zilizojitokeza kuhusiana na settings tuliweza kwa ushirikiano na
watengenezaji wa vifaa hivyo, kuzipatia suluhisho wakati zoezi
linaendelea. Pia chanagamoto za 'software' nazo zimekwishapatiwa
suluhisho. Changamoto kuhusu hardware zitarekebishwa wakati wa
utengenezaji wa BVR Kits 7,750 ambazo zilikuwa hazijaanza kutengenezwa
kusubiri matokeo ya zoezi hili la majaribio.
Marekebisho hayo ya hardware pia yatafanywa katika BVR Kits 250 zilizoletwa kwa ajili ya majaribio. Changamoto kuhusu fedha na lojistiki zinaendelea kushughulikiwa kwa ushirikiano na Serikali. Kuhusu changamoto za Watendaji tunaendelea kuzishughulikia kwa kuhakikisha Watendaji tutakaowatumia wanakuwa na utaalam unaotakiwa kuziendesha BVR Kits hizo.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Napenda pia niongelee baadhi ya masuala yanayohusu zoezi la Uboreshaji wa Majaribio kwa ujumla. Kwanza ni vyema ieleweke wazi kuwa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kwa ajili ya Kura ya Maoni ya Katiba Mpya, Mpiga Kura atatumia Kitambulisho cha Mpiga Kura alichopatiwa na Tume baada ya kuandikishwa katika mfumo huu tu na si vinginevyo. Vitambulisho vilivyotolewa katika uboreshaji huu wa majaribio ni vitambulisho halisi hivyo kila aliyejiandikisha katika zoezi hili la majaribio ni muhimu atunze kadi yake kwa ajili ya matumizi yaliyotajwa kwa kuwa taarifa zake tayari zimeingia katika Kanzi data ya Tume hivyo hataweza tena kujiandikisha kwa mara nyingine hata kama atabadilisha kituo cha kujiandikishia.

Pili, ni muhimu wananchi wakapata taarifa hizi kwa usahihi kwa vile wapo baadhi ya Watu wanaodhani kuwa kwa kuwa hilo lilikuwa ni zoezi la majaribio basi watakuwa na fursa nyingine ya kujiandikisha wakati wa zoezi la nchi nzima. Napenda nisisitize hapa kuwa kwa yeyote aliyejiandikisha katika zoezi hili, hatatakiwa tena kujiandikisha labda tu kwa yule ambaye atahitaji kubadilisha taarifa zake kutokana na sababu kama zilivyofafanuliwa na Tume.

Ndugu Wanahabari.
Napenda nisisitize pia kuwa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inayo dhamira ya dhati ya kukuza demokrasia kwa kuandaa na kuendesha chaguzi zake katika mazingira rafiki na wazi yatakayotoa fursa kwa kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 kutumia haki yake ya kikatiba ya kuchagua viongozi wake. Tume itakuwa tayari kupokea maoni na ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali
VICTOR SIMONNapenda nisisitize pia kuwa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inayo dhamira ya dhati ya kukuza demokrasia kwa kuandaa na kuendesha chaguzi zake katika mazingira rafiki na wazi yatakayotoa fursa kwa kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 kutumia haki yake ya kikatiba ya kuchagua viongozi wake. Tume itakuwa tayari kupokea maoni na ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali
No comments:
Post a Comment