Pages

January 11, 2015

Mchezo wa Nusu Fainali kati ya Polisi na Simba Uwanja wa Amaan Simba Imeshinda 1--0.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na wachezaji wa timu ya Simba kabla ya kuaza mchezo wa Nusu Fainali ya pili kati ya Simba na Polisi uliofanyika katika uwanja wa Amaan, Simba imeshinda bao 1--0, Itacheza fainali na timu ya Mtibwa baada ya kuitowa timu ya JKU kwa penenti 4--3.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akiwasalimia wachezaji wa timu ya Polisi kabla kuaza kwa mchezo wao na timu ya Simba.mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan
Kikosi cha timu ya Simba kilichoilaza timu ya JKU katika mchezo wa Nusu Fainal, uliofanyika uwanja wa Amaan.
Wachezaji wa Timu ya Polisi OLIwakiomba dua kabla ya mchezo wao kuaza wa Nusu Fainal uliofanyika uwanja wa Amaan, Timu ya Simba imeshinda bao 1--0.
Kikosi cha timu ya Polisi kilichopambana na timu ya Simba katika mchezo wa Nusu Fainali uliofanyika uwanja wa Amaan










Dk.Shein:Tofauti za Kisiasa na Vyama Zisitufanye Kukiuka Taratibu na Sheria za Kuendesha Shughuli za Kisiasa.

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                                                                 11 Januari, 2014
---
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza tena umuhimu wa viongozi wa kisiasa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa katika kuendesha shughuli zao za kisiasa na kuwa tofauti za vyama isiwe sababu ya viongozi hao kukiuka utaratibu na sheria hizo.
Akizungumza mara baada ya kupokea matembezi ya vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) katika viwanja vya Mnanzi Mmoja mjini Unguja jana ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Dk. Shein alisema kuwa “tofauti za kisiasa na vyama zisitufanye tukakiuka utaratibu wa kisheria uliowekwa”
Alibainisha kuwa Zanzibar inaendeshwa kwa misingi ya kidemokrasia kwa kufuata Katiba na sheria zilizopo huku kukiwa na vyombo vya kusimamia sheria na utoaji haki kwa kila mwananchi.
Dk. Shein ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar aliwakumbusha wanasiasa kutumia mfumo uliopo wa vyama vya vingi kushindana kwa sera na hoja na kuepuka maneno ya kuwatisha wananchi na kuwatia hofu.
Alibainisha kuwa kumekuwepo na ushirikiano mzuri katika uendeshaji wa Serikali iliyo chini ya mfumo wa Umoja wa Kitaifa hivyo kuhoji kulikoni baadhi ya viongozi wakiwa nje ya serikali wanafanya mambo tofauti.
“Tumekuwa tukishirikiana vyema katika serikali kulikoni huko? Kwa nini baadhi wanasahau utamaduni wa uongozi, lugha za viongozi na wajibu wao katika jamii”alihoji Dk. Shein.

No comments:

Post a Comment