Pages

January 2, 2015

KWA HERI 2014, KARIBU 2015: MIUNDOMBINU CHAKAVU YA MAJITAKA YAWATIBUA WANANCHI MORO, LISAA LIMOJA NA NUSU MANISPAA YAGEUKA BAHARI YA MAJI BARIDI NA MTO KIKUNDI.


Wakazi wa Manispaa ya Morogoro wakitembea kwenye maji ya mafuriko mtaa wa Madaraka wakati wakitoka eneo moja kwenda lingine desemba 31/ 2014.PICHA/MTANDA BLOG

Ajira ya muda, mwanaume akiwa amemeba mwanamke kwa makubaliano maalum mtaa wa Makongoro.

Ajira ya muda, mwanaume akiwa amemeba mwanamke kwa makubaliano maalum baada ya kusindwa kutembea katika maji ya mafuriko katika mtaa wa Makongoro.

Mwanaume wa jamii ya kifugaji akiwa na mke wake wakiwa katika makutano ya barabara ya Makongoro na John Mahenge wakivuka maji wakati wakisaka maduka ya kununua bidhaa.
Mkazi wa Manispaa ya Morogoro akitembea kwa tahadhali baada ya mtaa wa Makongoro kuzingirwa na maji ya mafuriko.
Mfanyabiashara wa kuuza ndizi mbivu akiwa ameduwaa baada ya eneo linatumika kuuza aina mbalimbali ya matunda, la kutokea magari soko kuu la mkoa wa Morogoro kujaa maji ya mafuriko.
Ni shida juu ya shida mafuriko yaliyovamia mitaa michache ya Manispaa ya Morogoro Desemba 31/ 2014
 Gari likipita mtaa wa John Mahenge kwa kutimua maji ya mafuriko
 Mwendesha pikipiki akiwa amekwama na abiria wake mtaa wa Makongoro.
Foleni ya magari jirani na daraja la mto Kikundi barabara ya Korogwe ikiwa imezingirwa na maji ya mafuriko na kusababisha eneo hilo kupitika kwa shida.
 Gari la hifadhi ya taifa ya Mikumi Morogoro likiwa limetumbukia katika mtaro mtaa waUhuru.
Mfanyabiashara Chandabay (katikati) akisaidiwa na ndugu zake kuyaondoa maji yaliyoingia dukani kwake mtaa wa Makongoro.
 Mwendesha pikipiki akitimua maji na kuzalisha mawimbi wakati akipita mtaa wa Makongoro
 Gari ndogo ikipita barabara ya Makongoro Manispaa ya Morogoro.
Soko kuu la mkoa wa Morogoro likiwa limevamiwa na mafuriko desemba 31/ 2014.

Na Habiba Yahya, Morogoro.Mvua kubwa iliyodumu kwa takribani saa moja na nusu mjini Morogoro jana, imeathiri miundombinu ya barabara na shughuli mbalimbali zikiwamo huduma za kijamii na biashara, kusimama.

Mvua hiyo iliyoanza kunyesha saa 5 asubuhi  hadi saa 6: 30 mchana, ilisababisha barabara za mitaa kadhaa ya katikati ya mji wa Morogoro kufurika kwa maji.

Hali hiyo iliathiri usafiri hasa kwa watu wanaotumia pikipiki maarufu kama bodaboda.
 
Barabara zilizoathirika zaidi ni pamoja na ile ya Kihonda kwenda katikati ya mjini na Barabara ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine kwenda Stendi ya Daladala.

Lakini pia eneo la stendi hiyo pia lilifurika kwa maji ambayo baadaye waliingia ndani ya magari.
 
Daladala zinazotoa huduma kati ya stendi hiyo na maeneo ya  Sua, Mazimbu na Kihonda zililazimika kusitisha shughuli za usafirishaji kwa muda kwa sababu barabara zilikuwa zimekufurika kwa maji na baadaye  foleni kubwa.

Katika eneo la  Kikundi ambako kuna mkondo wa maji, huduma za usafiri zilisimama baada ya wenye mgari kuhofia magari yao kusombwa
 
Mvua pia imesababisha kuvunjika kwa kuta za daraja lililopo katika Barabara ya Ahmadiya kuelekea Mtaa wa Ngoto.
.
Pamoja na mvua hiyo kuathiri  shughuli mbalimbali lakini ilikuwa neema kwa wauza miamvuli ambao walitumia fursa hiyo kufanya biashara yao mitaani.
 
Miamvuli hiyo ilikuzwa inauzwa kwa bei ya juu ikilinganishwa bei ya kawaida katika siku ambazo hazina mvua.

Mwamvuli mdogo ulikuwa ukiuzwa kwa bei ya kati ya Sh5,000 na Sh6,000 wakati kwa bei ya kawaida unauzwa kwa bei ya kati ya Sh2,500 Sh 3,000.

Miamvuli mikubwa ilikuwa inauzwa kwa bei ya kati ya Sh7, 000 na Sh8000 lakini bei yake ya  kawaida ni kati ya Sh 4,000  na Sh 5,000.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...