Naibu
Katibu Mkuu CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu akiutubia mkutano wa
hazara mjini Nansio Wilaya ya Ukerewe, Mwanza lengo kushukulu
wananchi kwa kukipatia ushindi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa
uliopita. Wilaya hiyo Chadema imepata viti 47 vya Serikali za vijiji
huku ccm ikipata 27 na CUF viwili.Ukerewe.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu amemsimamisha kazi
mjumbe wa kamati ya utendaji ya chama hicho Wilaya ya Ukerewe, Wilbrod
Machemli kwa kushindwa kutimiza wajibu wake, ikiwa ni pamoja na
kutotangaza ujio wa kiongozi huyo.Rungu hilo pia limemkuta katibu wa Chadema wilaya hiyo, Libelatus Mlebele ambaye amepewa onyo kali.
Akizungumzia
hatua hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Nansio jana,
Mwalimu ambaye ameanza ziara mkoani hapa juzi kwa lengo la kuwashukuru
wananchi baada ya kukichagua chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa, alisema hakuridhishwa na maandalizi yaliyofanywa na viongozi hao.
Kutokana
na hali hiyo, Mwalimu alimwagiza Mwenyekiti wa wilaya wa chama hicho,
Jacobo Munyaga kwa gharama zake amwandalie mkutano mwingine kabla ya
mwisho wa mwezi ujao.
Mwalimu pia alitilia shaka matumizi ya fedha yaliyotajwa kutumika kutangaza uwepo wa mkutano wake.
Alisema
Chadema hakipo tayari kulinda viongozi wazembe na wasiowajibika na
kuwaonya wajumbe wa kamati tendaji hasa katibu ambaye bado yupo katika
uangalizi wa miezi sita kwa maelezo kuwa anaweza kuondolewa kazini.
Kabla ya
kuchukua uamuzi huo, Mwalimu aliwaita mbele wakazi wanne wa kata za
Kakerege, Nansio, Nakatungulu na Kagera ambao walikiri kutosikia
matangazo ya ujio wake.
Hatua
hiyo aliichukua baada ya kuwasili katika Uwanja wa Mongera wa mjini
Nansio saa 9:30 alasiri huku kukiwa na idadi ndogo ya watu
ikilinganishwa na ziara zake za nyuma.
Mbali na
hilo, pia Mwalimu ametumia mkutano huo kukemea matumizi mabaya ya fedha
za serikali yanayofanywa na viongozi waandamizi wakati huduma za kijamii
zikizidi kuwa mbaya.
Alisema
ziara za mara kwa mara za nje ya nchi zisizo za lazima zinazofanywa na
Rais Jakaya Kikwete pamoja na viongozi wengine hazina tija kwa taifa.
Naye
mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Joseph Mkundi akizungumza
katika mkutano huo, alisema katika katika kipindi cha miaka minne ya
uongozi wao wamepata mafanikio makubwa.
Alisema
mbali na kusimamia vyema matumizi ya fedha za serikali katika
utekelezaji wa miradi ya maendeleo, pia halmashauri hiyo imekamilisha
mipango ya kununua greda moja la kutengeneza barabara lenye thamani ya
Sh400 milioni hivi karibuni chama hiko kimeluwa kikipigania
kukishinikiza serikali kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi.
Hata
hivyo, alisema mbali ya halmashauri hiyo kupata hati safi ya matumizi
ya fedha za umma pia hivi karibuni huko jijini Nairobi Kenya,
Halmashauri hiyo ilipata tuzo ya kukidhi vigezo vya sheria ya ununuzi ya
umma kati ya wilaya 166 za nchi nzima.
chanzo: gazeti la mwananchi
No comments:
Post a Comment