Jeshi
la wananchi wa Tanzania zaidi ya miatatu, wamefanikiwa kudhibiti sehemu
ya ardhi iliyobaki isiendelee kumezwa na maji ya bahari kwa kutumia
mawe na vifusi vya mchanga katika eneo la Msimbati lililopo Mtwara
vijijini.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika eneo la tukio kanali wa jeshi Saidi
Nkambi anayesimamia oparesheni hiyo amesema zoezi hilo linakwenda vizuri
na tatizo linalosumbua kwa sasa ni mifuko kwa ajili ya kujaza mchanga.
Kwa
upande wake kaimu mkuu wa mkoa Mtwara Ponsiano Nyama ametaka wananchi wa
mikoa ya Mtwara kuwa watulivu serikali inafanya kila juhudi kuhakikisha
dhoroba hiyo haileti madhara kwa mikoa ya Mtwara na Lindi, huku
muhandisi wa kiwanda kilichokaribu na bahari Peter John akiishukuru
serikali kwa hatua walizochukua.
No comments:
Post a Comment