Video ikiwaonyesha mateka wa Kijapan, Kenji Goto Jogo na Haruma
Yukawa, walio katika nguo za rangi ya chungwa, wakiwa na Jihadi John
anayedai fidia ya Dola milioni 200 ili kuwaachia mateka hao.
Mateka hao ni Kenji Goto Jogo mwandisi wa habari aliyekuwa anaandika
kuhusu vita vya ndani vya Syria mwaka jana, na Haruma Yukawa mwanajeshi
kutoka kampuni binafsi aliyekamatwa nchini Syria mwezi Agosti mwaka
jana.
Tishio hilo limekuja baada ya Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe,
kuahidi kutoa kiasi hichohicho cha fedha kama msaada usiokuwa wa
kijeshi kwa nchi zinazopigana dhidi ya ISIS.
Video hiyo iliyosambazwa katika tovuti zinazohusiana na wapiganaji
hao, ziliomwonyesha mpiganaji mwenye lafudhi ya Kiingereza ambaye
anajulikana kama ‘Jihadi John’ aliyeonekana katika video za mauaji ya
kuwakata vichwa mateka David Haines, Alan Henning (Waingereza), na
James Foley na Steven Sotloff (Wamarekani) hivi karibuni.



إرسال تعليق