Pages

January 2, 2015

Idara ya polisi yaongoza kwa ufisadi TZ


Jeshi la polisi nchini Tanzania ndio taasisi fisadi zaidi chini humo
Idara ya polisi ndio taasisi inayochukua hongo zaidi nchini Tanzania kulingana na ripoti ya ufisadi katika jumuiya ya Afrika mashariki.

Ripoti hiyo inasema kuwa maafisa wa polisi walipokea asilimia 25 ya hongo zote zilizotolewa kwa wafanyikazi wa taasisi za umma mwaka uliopita.

Ya pili ni idara ya mahakama,ambayo wafanyikazi wake walitia mfukoni asilimia 18 ya hongo,huku mashirika yalio na majukumu ya usajili na utoaji wa leseni yakiwa katika nafasi ya tatu kwa asilimia 10.

kwa mujibu wa gazeti la The Citizen, Idara ya Polisi nchini Tanzania imetajwa kuwa ya tatu kwa ufisadi katika jumuiya ya Afrika mashariki.

Polisi wa Uganda wanaongoza wakifuatiwa na wale wa Kenya katika nafasi ya pili na wale wa Burundi wakiwa katika nafasi ya nne.

Kulingana na ripoti hiyo maafisa wa polisi wa Rwanda ndio wasiochukua hongo ya juu Afrika mashariki.

Utafiti huo ulifanywa mwezi Julai na Agosti mwaka uliopita na shirika la lenye na maslahi ya kimaendeleo barani A
frika ForDIA likishirikiana na Jukwaa la uwazi nchini tanzania Trafo.

No comments:

Post a Comment