Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini, Profesa Norman Sigallah (aliyesimama)
akizungumza akifungua semina kwa ajasiriamali iliyofanyika kwenye ukumbi
wa Mtenda Sunset mjini Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini, Profesa Norman Sigallah akizungumza
akifungua semina kwa ajasiriamali iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mtenda
Sunset mjini Mbeya.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi akizungumza
katika semina kwa ajasiriamali iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mtenda
Sunset mjini Mbeya.
Baadhi ya wajasiriamali wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mtenda Sunset mjini Mbeya.
Baadhi ya wajasiriamali wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mtenda Sunset mjini Mbeya.
Baadhi ya wajasiriamali wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mtenda Sunset mjini Mbeya.
Baadhi ya Maofisa kutoka Benki ya Posta Tanzania (TPB) wakifuatilia mkutano huo.
Baadhi ya wajasiriamali wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mtenda Sunset mjini Mbeya.
BENKI
ya Posta Tanzania (TPB) Tawi la Mbeya, imetoa semina kwa Wajasiriamali
wa mkoa ikiwa na lengo la kuwaongezea ujuzi kwenye biashara zao. Semina
hiyo ya siku moja imefanyika kwenye ukumbi wa Mtenda Sunset mjini Mbeya
na kufunguliwa na Mkuu wa Wilaya, Profesa Norman Sigallah.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa semina hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi, Mkuu wa Wilaya
alitoa wito kwa wajisiriamali kutoogopa kukopa kwenye mabenki ili kukuza
mitaji yao na hatimae biashara zao.
Prof.
Sigallah alitoa changamoto kwa wajasiriamali kuhakikisha biashara zao
zinaubora unaotakiwa ili kuweza kujenga imani na ushindani kwenye soko.
Mkuu huyo wa Wilaya alitoa changamoto kwa benki ya Posta kuweka dawati
maalum la wataalam watakaotoa ushauri kwa wajasiriamali pindi wanapokuja
kuomba mikopo. Aliwashauri wajasiriamali kujiepusha na makundi yenye
muelekeo wa kuleta vurugu na kuvunja amani, kwani ili kukua biashara
yoyote inahitaji amani na utulivi.
Kwa
upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi,
akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wajasiriamali hao zaidi ya
150 waliohudhuria semina hiyo, alisema benki yake itaendelea kuboresha
huduma zake hasa upande wa mikopo, na pia kuangalia suala la riba
zinazotozwa kwa aina tofauti ya biashara.
"Benki
yangu itaendelea kuangalia ni namna gani tunaweza kuweka wataalam
watakaotoa ushauri mzuri kwa wajasiriamali ili kupunguza mlolongo mrefu
wa nenda rudi kwa mkopaji. Hii ni katika jitihada za kuhakikisha kuwa
mkopaji anapata mkopo kwa wakati ili kuwahi fursa iliyojitokeza,".
Akiongea
kwa niaba ya wajasiriamali hao, Bi. Joyce Mkongo, aliishukuru sana
benki ya Posta kwa kutoa mafunzo hayo kwao,ambayo yamewafungua macho na
kuwaondolewa woga wa kutumia huduma za kibenki. Alisema wajasiriamali
wengi wanasita kuchukua mikopo kwa hofu kuwa mali zao zitataifishwa
pindi watakaposhindwa kulipa mkopo.

Post a Comment