Pages

December 2, 2014

MHESHIMIWA ADAM MALIMA AFUNGUA MKUTANO WA UGAVI NA MANUNUZI LEO

Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima(kushoto)akisalimiana  na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya  Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB)Ahmed Kilima alipowasili jijini Arusha kufungua mkutano wa Siku mbili wa Wataalamu wa Ugavi nchini,wengine ni kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB,Clemence Tesha na Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Dk Hellen Bandio.

Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima akiongoza na maafisa wa  Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) katika mkutano wa  Siku mbili unaofanyika kwenye kituo cha mikutano cha AICC  jijini Arusha


Baadhi ya Maafisa Ugavi na Ununuzi wakisoma nyaraka mbalimbali za mkutano huo leo jijini Arusha.

Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima akisoma hotuba yake kwenye mkutano wa  Siku mbili  wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB)  unaofanyika kwenye kituo cha mikutano cha AICC  jijini Arusha.

Mkurugenzi Mtendaji wa  Bodi ya  Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB)Clemence  Tesha(kulia)akimpongeza Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima kwa hotuba nzuri.
Wataalam wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa AICC

Wataalamu wa Ugavi na Ununuzi nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Wazi wa Fedha,Adam Malima

 
Mwandishi wetu,Arusha
WIZARA ya Fedha, imeitaka Bodi ya Wataalam wa  Ugavi na Manunuzi nchni  (PSPTB), kutafuta ufumbuzi wa tatizo la kufanya manunuzi bila kuzingatia thamani halisi ya fedha na kuwataka waajiri kuacha mara moja  kuwaajiri watu wasio na sifa kufanya kazi hizo

Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima ametoa kauli hiyo leo  wakati akifungua mkutano wa tano wa mwaka wa Siku mbili unaofanyika kwenye jengo la Mikutano la AICC jijini Arusha ambapo aliwataka Wataalamu hao kuzingatia maadili na miiko ya kazi yao.

Amesema katika bajeti ya mwaka 2014/15 serikali imetega bajeti ya Sh trilioni 20 kati ya hizo asilimia 65 hadi za 70 zinatumika kwenye manunuzi ya bidhaa na huduma mbalimbali,hivyo taaluma hiyo kuwa na umuhimu wa kipee katika kudhibiti mapato ya serikali yasitumike vibaya.

Awali  Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Sr. Dk. Hellen Bandiho, amesema kauli mbiu ya mkutano huo “Thamani halisi ya fedha  za Manunuzi” ikilenga kuhakikisha serikali inapata huduma bora kulingana na fedha inazotumia ili kuinua uchumi wa nchi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...