MWANAMUZIKI
wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Nasib Abdul, Diamond
Platinum anashindana na aliekuwa mpenzi wake Wema Sepetu katika kuwania
Tuzo ya Mtu mwenye ushawishi mkubwa katika mitindo.
Tuzo
hiyo zitatolewa kwenye Onesho la Mavazi la Swahili Fashion 2014
linaloandaliwa na Kampuni ya 361 Degrees na zitatolewa siku ya mwisho
katika onesho la Swahili Fashion Week litakaloanza Desemba 5 hadi 7
mwaka huu.
Katika
shindano hilo wanaoshindana wengine ni pamoja na Mwamvita
Makamba ambae namba yake ya kupigiwa kura ni SFW SY 01,
Diamond Platnumz SFW SY 02, Millen Magesse SFW SY 03, Mohamed
Dewji SFW SY 04 na Wema Sepetu SFW SY 05.
Pia
Diamond anashindana katika kipengele cha wanaume wenye kuongoza huku
namba yake ya ushiriki ikiwa ni SFW SMP 01 na anaochuana nao katika
kipengele hicho ni pamoja na Luca Neghest SFW SMP 01, Baraka
Shelukindo SFW SMP 03, Noel Ndale SFW SMP, Rio
Paul SFW SMP 05 na Juma Juxx SFW SMP 06
Akizungumza
na waandishi wa habari mratibu wa tuzo hizo, Haruna Ibrahim alisema
kuwa kwa mwaka huu kuna ushindani mkubwa katika kila kipengele.
Aliongeza kuwa Meneja wa Msanii Wema Sepetu, Martin Kadinda nae anawania
kipengele cha Mbunifu bora wa mchango katika tasnia hiyo ambapo
anashindana na akina PSJ Couture SFW MWD 01.
No comments:
Post a Comment