Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,(
wa tatu kutoka kushoto) Naibu Rais wa Kenya, William Ruto, (kushoto
kwake) Makamu wa Rais kwanza wa Burundi, (kulia kwake) wakijumuika kwa
pamoja na viongozi wengine wakionyesha Taarifa ya pamoja waliyoisaini
kuhusu majadiliano ya kuimarisha Miundombinu kwa nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki, katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za
Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika kwenye Ukumbi wa
KICC, jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza katika mkutano wa tatu wa wakuu wa Nchi za Afrika
Mashariki (EAC) kuhusu miundombinu, uliofanyika katika ukumbi wa KICC
jijini Nairobi jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisaini taarifa ya pamoja ya majadiliano ya kuimarisha Miundombinu kwa
nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa mkutano wa 3 wa
Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu jijini
Nairobi, Kenya jana.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huyo kutoka nchini Tanzania......
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongozana na baadhi ya viongozi wakati wakitoka kwenye Ukumbi wa
mikutano wa KICC, baada ya kushiriki katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa
Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu uliofanyika jijini
Nairobi, Kenya jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine walioshiriki katika
mkutano huo.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akifurahia jambo na Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto na Waziri wa
Afrika Mashariki, Samuel Sitta, wakati wakiondoka katika viwanja vya
Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki kwenye mkutano wa 3 wa
Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika jijini Nairobi, Kenya jana.
No comments:
Post a Comment